![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
||||||||||||||||||||||||||||||
![]() |
||||||||||||||||||||||||||||||
![]() |
||||||||||||||||||||||||||||||
![]() |
||||||||||||||||||||||||||||||
Huruma Africares Foundation | ||||||||||||||||||||||||||||||
![]() |
||||||||||||||||||||||||||||||
Tribute: Red ribbon = fight against AIDS Pink ribbon = fight against Breast Cancer |
||||||||||||||||||||||||||||||
![]() |
||||||||||||||||||||||||||||||
LINKS: | ||||||||||||||||||||||||||||||
Tributes
• Mark of respect • Compliment • Honor • Praise • Acknowledgment • Accolade • Esteem • Homage |
||||||||||||||||||||||||||||||
![]() |
||||||||||||||||||||||||||||||
www.haftz.com www.haftz.com www.haftz.com www.haftz.com |
||||||||||||||||||||||||||||||
![]() ![]() |
||||||||||||||||||||||||||||||
TUMEHARIBU MAZINGIRA, SAYARI YETU SASA TABAANI | ||||||||||||||||||||||||||||||
MGONJWA katika hali mahututi. Ana matatizo mengi. Ana harufu mabya mdomoni. Ana homa kali sana. Jitihada za kumtibu haaifui dafu. Ana sumu mwilini. Anapotibiwa sehemu moja, ugonjwa unaibuka katika sehemu nyinigine za mwili. Kama angekuwa mgonjwa halisi, madaktaari wangesema ugonjwa wake ni atari na wa kutisha. Kwa kukosa la kufanya, wanejaribu tu kumtuliza kairi wawezavyo hadi saa yake ya kufa itakapowadia. Lakini mgonjwa huyo si mwanadamu. Ni makao yetu dunia. Mfano uliotajwa hapo juu unaeleza kinaganaga hali ya sayari yeti. Hewa chafu, ongezeko la joto duniani, maji machafu, na taka zenye sumu ni baadhi tu ya matatizo yanayoikumba dunia. Madaktari waliotajwa - wa mazingira, hawana la kufanaya. Kila wakati vyombo vya habari huandika kuhusu hali mabya ya dunia kupitia vichwa kama vile: 'Kuvuna samaki kwa baruti kwiangamiza habari', 'Huenda mabilioni ya Waasia wakakosa maji miaka 24 ijayo,' 'Tani milioni 40 za taka zenye sumu huuzwa ulimwenguni pote,' 'Karibu theluthi mbili ya visima 1,800 nchini...vina sumu', 'Shimo la tabaka la ozoni huko Antaktika lazidi, lasababisha wasiwasi,' nk. Watu fulani wamezoea kusikie habari nyingi kuhusu uharibifu wa mazingira na hata huenda wakadhai na kusema: "Si neon, maadam siathiriwi". Hata hivyo iwe twajua au hatujui, uharibifu mkubwa wa mzaingira ya nina, unaathiri watu wengi sana. Kwa kuwa sayri yaetu imeharibiwa san, yaelekea kwamba tayari maisha yetu yameathiriwa kwa kiasi kikubwa pia. Hivyo, sote twapaswa kuhangaikia hali ya makao yetu na jinsi ya kuyahifadhik. Tusipofanya hviyo, tutaishi wapi pengine? je, tatizo lenyewe ni bay kiasi gani? Dunia imeharibiwa kadiri gani? Watu wanaathiriwaje? Hebu tuchunguze mambo kadhaa yatakayotusaidia kuelewa, kwa nini dunia yetu iko katika hali mahutui. Bahari: Samaki wamevuliwa kupita kiasi katika sehemu kubwa za bahari. Ripoti moja ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa inasema kwamba, samaki wamepungua mno na hawawezi kuongezeka, hata wakizana kupita kiasi. Mfano mmojawapo ni kwamba, idadi ya aina mbalimbali za samaki katika bahari maendeo ya Atlanktiki Kaskazini, ikipungua kwa asilimia 95 kati ya mwaka wa 1989 na 1994. Hali hiyo ikiendelea, itakuwaje kwa mamilioni ya watu wanaotegemea bahari ili kuata chakula? Hata sato kwenye Ziwa Victoria wamepungua kwa asilimia 20. Isitoshe, inakadiriwa kwamba, kila mwaka tani milioni 20 hadi milioni 40 za viumbe wa baharini hukamatwa na kutupwa tena habarini kwa kawaida wakiwa wamejeruhiwa au wamekufa. kwa nini? Wao huvuliwa pamoja na samaki, lakini baada ya kuvuliwa, hugundulika kwamba hawahitajiwi. Uharibifu wa misitu una athari nyingi. Ukatili kwa miti upunguza uwezo wa dunia wa kufyonza hewa ya ukaa, na inasemekana kwamba, jambo hilo linasababisha ongezeko la joto duniani. Aina fulani za mimea ambazo zinaweza kutumiwa kutengeneza dawa muhimu zitatokomea. Hata hviyo, misitu inaendelea kukatwa ovyo. Ama kwa hakika, misitu inaendelea kuharibiwa kwa kiwango kikubwa sana katika miaka ya karibui. Wataalamu wanahisi kwamba hali hiyo ikiendelea, misitu ya Kitropiki inaweza kuangamia kaika muda wa miaka 20 tu! Kutupa taka hatari kwenye nchi kavu na baharini, ni tatizo kubwa linaloweza kudhuru mamilioni ya watu kwa kiasi kikubwa. Taka zenye manuru, vyuma vizito na plastiki, ni baadhi ya vitu vinavyo weza kusababisha ulemavu, magonjwa, au kifo kwa watu na wanyama. Tumeshudia kwa kipindi cha miaka 10, meli kubwa zikimwaga mafuta kwanye maziwa na bahari zetu. Katika miaka 100 iliyopita, karibu aina 100 za kemikali zilianza kutumiwa. Kemikali hizo husambaa kwenye hewa, udongo maji, na katika chakula. Ni kemikali chache tu kati hizo amabazo zimechunguzwa ili ijulikane kama zinadhuru wanadamu. Hata hivyo, kemikali nyingi kati zile zilizochunguzwa, zimegunduliwa kuwa zinaweza kusababisha kansa au magonjwa mengine. Kuna vitu vingi zaidi vinavyo hatarisha maisha yetu, navyo ni uchafuzi wa hewa, maji machafu, mvua ya asidi, na ukosefu wa maji safi. Mambo hayo machache yanaonyesha wazi kwamba dunia yetu iko katika hali ya umahututi. Je mgonjwa huyo anaweza kuokolewa, au tumechelewa mno? Chernoby1 Bihopal, Valdez, kisiwa cha freemail. Majina hayo hutukumbusha misiba ya kimazingira iliyotokea katika sehemu mablimbali za ulimwengu. Kila moja ya misiba hiyo, ilitukumbusha kwamba mazingira ya dunia yanaharibiwa. Wataalamu na watu wengine mmoja mmoja, wameelezea wasiwasi wao. Wengine wamechukua hatua za waziwazi kuonyesha msimamo wao. Mwingereza mmoja ambaye ni mhudumu wa maktaba, alijifungia kwenye tingatinga kwa mnyororo, ili kupinga ujenzi wa barabara katika enoe lake, ili kubabili uharibifu wa mazingira. Wanawake wawili Waaborigini huko Australia, waliongoza kampeni ya kupinga uchimbaji madini ya urani katika mbuga ya taifa. Shughuli hizo zilisimamaishwa kwa muda. Japokuwa jitihada hizo hufanywa kwa nia nzuri, mara nyingi hazipendwi na hupigwa vitra, kumbe ni katika kuboresha mazingira yetu. Kwa mfano, nahodha wa jeshi la wanamaji katika Serikali ya Sovieti, alihangaishwa sana na minururisho iliyokuwa ikivuja kutoka kwenye mitambo ya nyambizi za nyukilia iliyozama. Alipochapisha habari kuhusu maeneo ambapo nyambizi hizo zilikuwa, alikamatwa. Masharika mablimbali pia yameonya kuhusu hatari zinazoyakumba mazingira. Mashariki hayo ni kama vile Shirika la umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira na shirika la Green Peace. Hata hivyo, baadhi ya mashirika hayo huripoti tu. kuhusu uharibifu mazingira unaohusiana a kazi zao. Mengine hujitoa mhaga kutetea mazingira. Shirika la Green Peace linajulikana kamatika kutumia wanaharakati kwenye maeneo yaliyokuwa na matatizo ya mazingira, na matatizo ya mazingira na kuufahmisha umma kuhusu masuala kama kama vile ongezeko la joto duniani, na hatari za wanyama na mimea iliyobadilisha chembe ya urithi. Wanaharakati wengine husema wao hubuni njia za kutangaza uharibifu wa mazingira ulimenguni kote, ndiyo sababu wengine hujifungulia kwenye milango ya mashine za kupasulia mbao, wakipinga uharibifu wa misitu ambayo imekuwapo siku nyingi. Kikundi kimoja cha wanaharakati kilizusha zogo, nchi moja ilipovunja mkataba wa kuvua nyangumi. Waaharakati walifika kwenye ofisi za ubalozi wakiwa wamevalia vinyago vyenye macho makubwa, ili kuonyesha kwamba matendo ya nchi hiyo yalikuwa yanatazamwa. Matatizo ya mazingira ni mengi.Kwa mfano, watu na mashirika ni mengi kwa mfano, watu na mashirika wameonya mara nyingi kuhusu uchafuzi wa maji. Hata hivyo, hali ni mbaya sana. Watu milion 3.4 hufa kila mwaka kutokana na magonjwa yanayoambukizwa kupitia maji," Gazeti la Time liliripoti. Tatizo jingine ni uchafuzi wa hewa, kama ilivyoripotiwa kwenye Jarida la State of World Population 2001, likisema uchafuzi wa hewa hudhuru watu zaidi ya bilioni 1.1 Likaripoti kwamba, karibu asilimia 10 ya magonjwa ya kupumua yanayowapta watoto katika Ulaya, husababishwa a uchafuzi mdogo sana. Naam, licha ya maonyo na hatua zilizochukuliwa hadi sasa, matatizo yanyoathiri mambo ya msingi maishai yamezidi. Watu wengi wamechanganyikiwa. Habari nyingi zaidi kuhusu masuala ya mazingira, zinapatikana sasa kuliko wakti mwingine wowote. Watu wengi na mashirika mengi, wana nia ya kusafisha mazingira kuliko wakati wowote. Serikali zimeanzisha idara za kutatua matatizo hayo. Tuna teknolojia ya hali ya juu zaidi wakati huu, ya kusaidia kukabiliana na matatizo hayajaboreka. kwa nini? Tutaona wiki ijayo.. |
||||||||||||||||||||||||||||||
Nunua gazeti la ........... kupata zaidi |