TOP

PAGE 5

I Previous page I Full page List I Next page


Hadithi tatu za Buddha; Tafsiri ya Kiswahili.

From: Three unknown Buddhist stories in an Arabic Version:( text, with English translation by S.M.Stern and Sofie Walzer, published by Bruno Cassirer, Oxford, 1971/1390).

Hadithi tatu zisiojulikana katika kitafsiri kiarabu: (maandiko, pamoja na tafsiri katika lugha ya kiingereza) kilichochapwa na Bruno Cassirer, Oxford, 1971AD/1390AH.


Bowl : Northeastern Iran or Transoxiana, tenth century AD/third century AH, Earthenware; Bakuli la ufinyanzi wa udongo, Iran ya Kaskazini au Transoxiania, karne 10 ya kristo/3 ya hegira. © Los Angeles County Museum of Art
Dibaji

Hadithi hizi tatu, ambazo zinatuonyesha njia zilizopita habari za Buddha kutoka Uhindi mpaka nchi za Wilaya, ni za kutustaajabisha pia kwa sababu nyingi.

Kwanza, mifano wa hekaya hizi ziliandikwa katika Kifarsi cha zamani sana, na hizo zilitafsiriwa, na ziliandikwa katika Kiarabu na mwandishi asiye na tufahamu sasa , mnamo karne ya nane ya Kristo, au ya pili ya hegira. Maandiko haya yalitafsiriwa tena katika lugha ya Kijurji. Kufuatana na hiyo, hadithi ziliendelea kua za Kikristo, na katika lugha ya Griki, nakili yake ilitimiza kama kisa kamili cha Kikristo Ugriki, yaani 'Joasaph na Barlaam'. Mwandishi wake alidaiiwa kuwa Saint John ya Damascus, aliyefariki katika zamani zile. Lakini, ni wazi kwamba nakili ya Griki siyo ya wakati ule, na ilitafsiriwa kwa kutumia ile ya Kijurji miaka mengi baadaye. Tena, katika kitafsiri Kiarabu hamna lolote la Kikristo, lakini katika cha Kijurji, liko chanzo chake, ambacho kiliongezwa bila shaka katika kitafsiri Kigriki. Kwa njia hii, Buddha na mwalimu wake, Budasf na Balawhar, walibadilishwa kuwa Joasaph na Barlaam, mitume wa Kristo kwenda Uhindi. Kama dhana hii ni sawa, kitabu hicho cha Kiarabu, kilichoitwa 'Balawhar na Budasf', ni asili ya visa vyote vyingine, hasa kwa sababu kile katika lugha ya Kifarsi cha zamani kimepotea.

Halafu, humu ndani kitabu ya Ibn Babuya, mwislamu, na mwarifu wa dini katika karne ya kumi kristo, au nne ya hegira, zimo hadithi tatu. Hizi tatu ni hadithi zimezotafsiriwa hapa chini. Waalimu wa maandiko ya zamani hawajui kwa hakika kwamba hadithi hizo tatu ziliongezwa na nyinginezo baadaye, au mwandishi mwenyewe aliandama hizo chenye kitabu chake. Viandiko vilivyotumikiwa kufasiri hadithi hizo tatu hapa ni vya vitabu viwili.

Cha kwanza ni kitabu cha Ibn Babuya, 'Kamal ad-Din wa Tamam al-Ni'ma (Ujazi wa Dini na Timamu ya Neema)'. Hicho ni kitabu cha Balawhar na Budasf katika lugha ya Kiarabu. Cha pili ni tafsiri ya Aqa Muhammad Baqir (Majlisi) katika kitabu chake cha karne wa kumi na saba ya Kristo, na kumi na moja ya hegira,'Bihar-al-Anwar ( Bahari ya Uangavu)', ambacho ni kitabu kikubwa, na kamusi ya Waislamu Washia. Asili ya hadithi hizo tatu katika kitabu hiki cha pili zinathabitishwa zaidi na nyinginezo katika lugha ya Kifarsi, zilizotafsiriwa na Majlisi katika kitabu chake jina la 'Ain al Hayat (Chemchemi cha Maisha)'.

Jambo lingine ni kuhusu jinsi ya maandiko haya katika lugha ya Kiarabu. Namna ya kutumia Kiarabu siyo chepesi, na pengine kigeni, hata kinalazimisha kazo la fikira nyingi kukielewa. Labda tafsiri ifuatayo, ingapo inaonekana hivyo, ni kwa sababu hiyo, lakini makosa mengine mengi bila shaka ni ya mfasiri mwenyewe, na hapo anaomba msomaji amsamehe.

I. Hadithi ya unwyele wa mfalme mvi.

Inadaiwa kwamba kulikuwa mfalme zamani aliyeisifiwa elimu yake, mpole, na wa siasa, aliyependa adili kushinda juu ya watu wake, na suluhu kuenea katika waraia wake. Aliishi hivyo kwa muda pamoja na hali nzuri. Halafu, akafa, na watu wake walimlilia matangani. Mwanaamke mmoja wake alikuwa na mimba, na manajamu na makahini waliagua atakuwa na mtoto mwanaume. Aliendelea kuwa msimamizi wa utawala yule mwenyewe aliyeuongoza wakati wa mfalme wao. Na ilitukia kama walisema hawa sote wawili , manajamu na makahini, na alizaliwa kutokana na mimba mtoto mwanaume. Ilisimikwa baada ya siku ya kuzaliwa yake, mwaka moja wa muziki, wa kujifurahisha, wa kukunywa na kukula.

Baadaye, waalimu, makasisi, na watu wa dini walisema kwa wajamaa wao: " Ikiwa mzaliwa huyu ni hiba ya Mwenyezi Mungu, nyinyi mmeshukuru mwinginiye; lakini ikiwa hiba asiye kutoka Mwenyezi Mungu, mmelipa haki kwa yeye aliyewampa, na mmeonyesha juhudi ya kutoa shukrani kwa yeye aliyewamriziki." Watu walijibu kwao, "Hajatutuza sisi yeye ila Mungu bariki na Mwenyezi." Waalimu walisema," Kama ni Mungu Mwenyezi aliyewahebu yeye, nyinyi mmeridhisha mwingine na yule aliyewampa na mmekasirisha Mungu ndiyo aliyewampa." Waraia walisema kwao, "Kama ni hivyo, fanya shauri na sisi , nyinyi wa hekima, na tupe habari ilivyo, nyinyi waalimu, tufuatayo maneno yenu, na tukubali na nasaha yenu. Toeni amri tuishike." Waalimu wakajibu: " Sisi tumewaza mjiongoze kwa kutoridhisha shetani na kucheza muziki, na kujifurahisha , na kurusha akili yenu, na badili yake kujaribu kuridhisha Mungu Mwenyezi, na kumshukuru yeye maradufu kuliko shukrani zao kwa shetani, hatimaye, aweze kuwasamehe." Waraia wakanena, " Haitaweza kuhimili miili yetu yote mnayotuambia na mnatuamuru kuifanya." Waalimu wakanena," E nyinyi washenzi. Mliwezaje kutii asiye na haki kwenu, na mnaasia yeye anayehaki wajibu juu nyinyi. Mmepataje uwezo wa kutenda vile havipaswi kutenda, na sasa kutokuwa na nguvu kufanya vile vingefaa kutendwa?" Walijibu kwao, " E viongzi wa hekimu, shauku zetu zilikuwa nyingi, na uchu uliongezeka hata nguvu tulizopata nazo ilikuza zilizokuwa ndani zetu, na ilidhoofisha nia zote zetu; hata sasa, hatuwezi kuhimili vile vizito. Watupe radhi turejee siku kwa siku na msitupagaze mizigo hii yote." Walisema kwao, " E wajamii wapumbavu. Si nyinyi watoto wa ujahili, na ndugu wa ukosefu, kuwaona unyonge wepesi, na wema mzito ?" Walisema hao," E mabwana za hekima , na viongozi wa elimu. Kwa makiripio yenu tutakimbilia Mungu Mwenyezi na Mwenye sifa atughofire, na kwa maneneo yenu yatatusetiri masamaha yake. Msikemee sisi wala msituambilie udhaifu wetu, au kuaibisha ujahili wetu kwetu. Maana, tujapotii Mungu, mwenye masamaha na ulaini, na marudio marudufu ya uzuri , na kujitahidi kufanya ibada yake kwa kadiri tulivyofuata ngoa ovyo zetu, tutajipatia mahitaji yetu, na Mungu Mwenyezi atatusaidia tupate makusudi yetu kwa kutuonyesha rehema kama ndiye aliyetuumba." Wakinena hivyo, waalimu wao walikubali nao na makauli yao yaliwafurahisha. Walisali, na walifunga, na waliabudu, na waliongeza sadaka hata mwisho wa mwaka mmoja.

Ulipokwisha muda huu makahani wakasema, " Kwa ajili ya vile vimevyotenda wajamii hao kwa mzaliwa huyu, inakupa habari kwamba mfalme huyu atakuwa mbaya, na atakuwa mwema, atakuwa mkorofi na atakuwa mnyenyekevu, na atakuwa mwovu na atakuwa mzuri." Makahina walinena hivi vile vile. Waliambiwa, "Mnawezaje sema hivyo?" Manajimu walisema , "Tumesema hivyo kwa sababu ya michezo, na muziki, na vyote vya ovyo vilivyofanyikiwa kwake na , tena, vilivyofanyikiwa juu yake baadaye." Na manajimu walisema, "Tumesema hivyo kwa kuwa ulingano wa enzi ya Zahara na Mshtarii"(1).

Mtoto alipevuka, na alijipigia kiburi ukubwa wake hausifiwi, na alijichangamka jinsi haipimwi, na ubishi haufumbatwi.Tena, alikuwa mkali, mjeuri, na mdhulumu wa hukumu, tena mkorofi, na alipenda watu wale waliopatana naye, na alichukia na wao waliohitalifiana naye. Ujana wake ulimdanganya yeye, pamoja na siha, kudura, ushangwe, na ushindi wake. Alijijalia furaha na alijivuna, na aliona kila alivyotaka, na alisikia kila alivyopenda mpaka alifika miaka thelathini na mbili.

Halafu, alisanya wanawake wa wasichana wa wafalme, na wavulana, na vijakazi waliotengwa, na farasi wake wa asili bora na safi, na namna za marekebu wenye fahari, na watumishi wake, wake kwa waume, waliohudumu yeye, na aliwaamuru wavae nguo zao mpya , na wajipambe mapambo mazuri yao. Alifanya amri wajenge chumba kubwa sawa na uche wa jua. Sakafu ya ardhi iwe ya dhahabu, na kazi ya njumu, na zitiliwe johari za rangi mbali-mbali. Urefu wake uwe dhiraa mia na ishirini, na upana, dhiraa sitini, na hata sakafu na kuta zirembeshwe kwa kutumia uzuri wa vito vya karimu, na lulu za fahari. Aliamuru, tena, ziletwe aina za mali, zikatolewa zile zilikuwamo hazinani na zilipangwa kwa safu mbili mbele ya mkutano wake. Aliamuru jeshi lake, waandani wake, viongozi wake, waandishi wake, mabawabu wake na pia wakuu na waalimu wa nchi yake. Na hawa wote walihudhuria katika sura nzuri sana mno , na jamala bora mno iliyowezekana. Wapanda farasi walitwaa silaha na idadi za vikundi vya farasi wa jeshi walipiga mwendo. Baadaye, walisimama katika mipango na mistari yao, kwa safu na jamii. Kwa vile, nia yake ilikuwa kuona mandhari ya urembo ukubwa kufurahishia moyo wake , na wonyesho wa kupendezwa na macho yake. Hata alitoka, na alipanda pale penye mkutano wake na alitazama juu ya milki yake, na wote walimlalama na wakamsujudu.

Halafu, alisema kwa ghulamu: "Sasa nimeona mamlaka yangu kwa mandhari nzuri, na imebakia kuutazama uso wango mwenyewe." Aliagiza kioo na alijitazamia uso wake, na katikati ya kugeuza macho humo , mara ulionekana kwake unywele mweupe ndevuni kama kunguru mweupe miongoni mwa kunguru weusi. Utisho na hofu ukubwa ulimogofya yeye kwa vile, na kwa maoni yake, hali yake yote ilikuwa imebadilika, na ilionekana huzuni na uzito katika sura yake, na ondokeo la furaha yake. Baadaye alinena kwa mwenyewe, " Huu ni wakati wa tangazo la kifo cha ujana wangu kwangu, unapambazua chweo la miliki yangu karibu, na unanipa habari nishukie kiti cha kifalme." Akasema tena, "Huu ni umbele wa mauti, na ujumbe wa uozi, ambao haukuweza mbawabu wangu kuzuia, wala mlinzi wangu kupingia kwa mimi. Inaletea utangulizi wa mwisho wangu , na upotezo wa ufalme wangu. Mbona upesi huu wa kugeusha ukunjufu wangu, na kuondosha ufurahifu wangu, na kuangamiza nguvu yangu! Hakuwa na boma iliyoweza kunihifadhia kwake, wala jeshi lililoweza kuufukuza. Huu, huyu, ni mvivi wa ushababi na uwezo, na mfutwa wa enzi na mali, ambaye anafumua umoja, na anafarikisha urithi hata kwa marafiki na maadui pamoja. Ni mwozi wa maisha, na mwangamizi wa ladhaa, mharabu wa majenzi, na mtenga wa ujamii, ni mshushi wa mwanacheo, mtwezi wa nguvu. Uzito wake umenikunjisha, na nyugwe zake zimewekea mtambo wangu." Halafu, akatelemka kwa mkutano wake bila viatu, na kwa miguu mitupu, kumbe mbele alipanda juu kwa kubebwa.

Baadaye, alisanyika majeshi yake, na aliitia kwake waandani wake, na akasema, " Wazee wangu, Nimefanya kwenu nini? Na nimewapa nini kwenu tangu nilitawala nyinyi na nilihukumu nyinyi?" Wao walisema, " E Mfalme wetu mshindi. Ushujaa wako mkubwa kwetu, na tuko tayari sisi kutii wewe hata na maisha yetu. Toa amri, tu.!" Yeye alisema," Mwadui wa kumcha amepiga hodi mlangoni wangu, na nyinyi hawakuweza kumepusha yeye hata amenishika, na nyinyi ndiyo walinzi na waamana wangu."

Hawa walisema," E Mfalme, Huyu mwadui ni wapi? Aonekana yeye au haonekani?" Alisema, " Athiri yake huonekana lakini yeye mwenyewe haonekani." Walisema, " Ewe Mfalme! Huu ni utayari wetu kama unavyouona, na pa sisi utulivu, tena miongoni wetu tuna wao wanazo akili na ujuzi. Tutamfaa wewe kama yeye alikutoshea." Alisema, " Ghururi yangu, kutokana na nyinyi, imezidi kweli, na niliweka amani yangu pasipokuwa mahali pake wakati nilipochagua nyinyi nakuwawekea kama ngao yangu. Kwa kweli, nimetumia mali tele kwenu, nimepandisha vyeo vyenu, na nimesimamisha nyinyi wawe waandani wangu kuliko wengineo, kunihifadhie kwa waadui wangu na kunilindia kwao. Tena, nimewasaidia kuifanya ile kwa kuundisha ujenzi, na kuhusunisha miji, na kutegemeza na silaha zenu. Nimeuondoa usumbufu wenu, na nimewaachia kufanyana kazi ya msaada na tunzo. Sikukuwa na wasiwasi ya mshtuko nilipokuwamo nanyi, wala sijaogopa ajali mwilini, wakati mlishughulika kunizingia. Kumbe nimejiwa, na nyinyi wapo pande zote, na nimefikiwa, na nyinyi baado nami. Ingawa hii ilikuwa udhaifu wenu, amri yangu haikukuwa sawa kuwaamini, na kama ilikuwa nyinyi kutoniangazia basi nyinyi sio wenye uonyo, na mimi sina wenzangu."

Hawa walisema," Ijapokuwa tutaweza kukiepusha kile na farasi au nguvu, hakitaweza kukufikia kwako, inshaallah, kwa muda tuko hai. Lakini, kile ambacho haonekani, na cha kile kimechoghibia hatuna ujuzi, na nguvu zetu hazifai kwake." Yeye alisema, "Nimewateuaje, isipokuwa kuniwekea salama kwa maadui wangu? " Walijibu, " Naam!" Alisema," Kwa adui gani mtanihifadhia? Kwa yeye ananiumiza au yule asiye kuniumiza?" Walijibu, "Kwa yeye anakuumiza." Aliendelea kusema, " Kwa maumizi yote, au kwa baadhi tu?" Walijibu, "Kwa maumizi yote." Alisema yeye, "Mjumbe wa balaa amekuja kwangu kuniambia habari ya kifo changu na cha miliki yangu, na amedai ataharibu vile nimevyojenga, na atavunja vile nimevyosimamisha. Vile vile faraka vya vile nimevyoungisha, uovu wa vile nimevyosuluhu, tawanyiko ya vile nimevyopatia, badala ya vile nimevyotendea, na ulegeo wa vile nimevyothabiti. Tena, anajigamba anaye shamata za maadui wameofurahisha mno kwa kuniona machoni, na anajifikiria wape hao ridhaa moyoni kutokana na mimi. Amenena pia atashinda juu ya majeshi yangu, ataniweka mkiwa kwa kujuana, ataiba ukuu wangu, atayatamu watoto wangu, atatengua jumuiya yangu, na kwa ajili yangu atawasumbua ndugu na ahali na karibu zangu, mpaka amekata viungo vyangu vyote, na penye makao yangu amekalisha waadui wangu."

Walisema hawa," Ewe Mfalme! Tunao yakuhifadhia na watu, au wanyama wa mwitu, au wadudu, au watambazi wako duniani, lakini hatuna uwezo juu ya wozo, wala nguvu kuushinda, wala kukupingamisha nao hatuna." Alisema yeye, "Yuko hila kuufukuza ule kwangu?" Walisema, "La!". Aliwauliza, " Je, duni yake mnayo uwezo ?" Walisema, " Maana yako nini ?" Alisema yeye, " Umivu, huzuni na hamu." Walisema, " Ewe, Mfalme! Kudura ya Mungu mwenye enzi na latifu ameziumba hizo. Inavumbilia mwilini na kwa nafsi, na inakufikia bila kufikika wewe, Haifichishi kwako na ikiwa mfichaji haifichami." Alisema, "Na jambo ambalo ni ndogo lake?" Waliuliza, "Na nini hilo?" Alisema, " Neno limelotanguliwa." Walisema hawa, " Ewe Mfalme! Nani ambaye ameishinda desturi bila kushindwa mwenyewe, na nani kubwa yake hakuweza kufaulu naye?" Alisema, " Basi, mnao nini?" Walisema, " Hatuwezi kukukingiza na ajali. Wewe umekwisha pata fanaka na nasibu, unataka nini zaidi?" Alisema," Nataka rafiki wawe uaminifu daima, na waniamini, na wanao undugu wa kubaki na wasichukuliwe na mauti, wala wakatazwe na wozo kusuhubiana nami, au wawe na tamaa inayoweza kutonasihi mimi, au kufarikiana nami ingawa nife, au kuniacha na mimi baado yu hai, na pia kuniepushia vile vyote ambavyo nyinyi hawakuweza,kuhusiana na mauti." Walisema hawa, " Ewe Mfalme! Na nani hao unayoelekea?" Alisema, "Ni wale nimewafisidi kukuwa mzuri kwenu." Walisema, " Ewe Mfalme! Hutaweza kufanya maarifa na sisi sote wawili, maana hulka yako ni timamu, na upole wako mkubwa?" Alijibu yeye, " Usuhuba yenu sumu katili, utii wenu ni upofu na uziwi, na kuafikiana na nyinyi ububu." Hawa waliuliza , "Na hivyo kwa nini?" Alisema, " Kwa kuwa urafiki wangu kwenu ni maongezo ya mali, na kuafikiana nami mapatano, na utii wenu na mimi nikutofanya lolote. Mmenikawilisha kufika ahera, na mmerembesha dunia kwangu. Ningependa mngalinasihi mimi na ukumbusho wa mauti, na mngalihurumia nami. Au mngekufahamisha mimi na wozo, au kusanya yale ambayo hayana ukomo, na hamngaliongeza yale yakupotea. Kwa sababu zote hizo manufaa yote yadaiwa na nyinyi ni dhara, na upendo ule, ushindani. Nayarudisha kwenu, sina haja nayo kwa nyinyi."

Hawa walisema," Ewe Mfalme, Mwenye hekima na kuhimidiwa, tumeelewa kauli zako, na katika nafsi zetu tunalo jibu, isipokuwa hatufai sisi kuhoji nawe na tumekwisha ona mahali pakuhoja, lakini kunyamaza kimya kwa kutotoa hoja zetu nikuangamiza miliki yetu. Ni mwisho wa dunia yetu, na shamata ya maadui yetu. Hii, badala ya rai yako, na kukata shauri hivyo limekuwa jambo kubwa letu." Alisema yeye," Msemeni kwa amani, na mleteni mawazo yenu bila hofu. Mimi mpaka siku hii nilikuwa nimeshindwa na kichocheo na kiburi, leo nimevishinda, na mpaka siku hii nilikuwa nimeghilibiwa na hivi viwili, leo nimeghilibu juu ya sote mbili, na mpaka siku hii nilikuwa mfalme katika utawala wenu, lakini leo nimepata huru. Leo nyinyi waliokuwa chini ya kifalme changu wametolewa utumwani." Walisema hawa," Ewe Mfalme! Ulikuwa mtumwa wa nani wakati ulikuwa mfalme wetu?" Alijibu yeye, " Nilikuwa mtumwaji wa shauku, na mshinde wa ujuhula, na mwabudu wa mashawishi yangu. Nimekata utii huu kwangu, na nimeutupa nyuma ya mgongo wangu." Walinena, " Sema umeloamua, Ewe Mfalme!" Aliwaambia, " Niwe mkinai na kujiuzulu hata aheri yangu. Kuachia udanganyifu huu, kurusha mzigo mgongoni wangu, na kujitayarisha kwa ufu na kujiiandaa kwa wozo vile vile. Mjumbe wake amekwisha nipa habari kwamba ameamuriwa aambatane nami, na akae nami, mpaka nipitiwe na mauti." Walisema, " Ewe Mfalme! Ni Nani huyu mjumbe aliyefika wewe na sisi hatukumwona, huyu aliyekuwa mtangulizi wa ufu na sisi hakutumjua?" Yeye alijibu, " Mjumbe alikuwa mweupe huu ulitokeamo miongoni mwa ueusi, Kwa wote wengine analia mwisho ambao wengineo wanaitikiana, na wananyenyekea. Mtangulizi wa ufu ni wozo, na unywele mweupe huu ni mwanzo wake."

Walisema hawa, " Ewe Mfalme! Kwa nini unawaachia watawaliwa wako, na kutoangalia waraia wako? Mbona huogopi dhambi ya uvivu na wajamii wako? Kwani hujui kwamba zawadi kubwa kuliko zote ni kusuluhisha watu, na upeo wa wema nikutii wajamii na watu? Unawezaje kutoogopa dhambi, maana uangamizi wa ujamaa ni dhambi zaidi kuliko taraja ya ile utajistahilisha kwa kujiongoza mwenyewe? Hujaelewa baado kwamba ibada nzuri kuliko zote ni utendaji, na utendaji bora kuliko wote ni siasa? Na wewe, Mfalme, ni adili kwa waraia wako, tena bila shaka mwongozi wao kwa usimamizi wako, na ni wewe ndiyo utapata zawadi kadiri umevyowaongoza? Ewe Mfalme! Siyo kufikiri fisadi zao kutosuluhu jamia ya watu wako wapo mbele yako ? Maana, kwa kutaka fisadi zao umekwisha letea juu yako dhambi zaidi kuliko unaweza kujipatia kwa kuangalia mwenyewe. Ewe Mfalme, umesahau kwamba waalimu wasema: ' Ameyodhuru mwingine huwajibisha dhara mwenyewe, na ameyosuluhu mwingine, huwajibisha suluhu mwenyewe'? Ufisadi upi kuhusiana na watu wote ni zaidi kuliko kukana waraia hawa, na kiongozi wao ambao ni wewe? Na usuluhi upi (kuhusiana na watu wote) huzidi kikao cha umma hiyo, na mtungaji wao ambao ni wewe? Hasha wewe, Ewe Mfalme, uvue nguo za kifalme chako ambazo ni njia ya usharifu duniani, na ahera pia!"

Alisema yeye, " Nimekwisha fahamu mnayosema, na nimeelewa mnayoniambia. Na ijapokuwa mimi nilitaka kuuletea ufalme juu yenu kufanyia haki kwenu ili nijipatie zawadi ya Mungu, na kuwaongoza bila kutegemewa na auni zenu, au bila mawaziri wa kutosha, ningeweza kujifikiza mpaka wapi kwa upekee wangu? Kwani nyinyi nyote hamna tamaa ya dunia, na shauku, na ladhaa? Na mimi sina yakini sitakupotea duniani, badala ya kutumaini niiachie mbali, na nikanushe. Na nikifanya hivyo, na ningalichukuliwa na kifo kwa ghafula. ningeanguliwa kwenye kiti cha kifalme changu hata kuingiwa tumboni mwa ardhi, na hapa kupakwa na udongo baada ya dibaji(2), mfumo wa dhahabu, na johari bila thamani. Halafu, ningetiliwa penye pembamba kuliko papo upana, na ningevalishwa kinyonge baada ya karama, na ningekuwa na mimi na upweke, bila nyonyote nami. Nyinyi mmenitokeza kwa ustaarabu na mmenisalimisha pa uharibifu , tena mmeniachia nyama ya mwili wangu miongoni mwa ndege wakatili, na madudu wa ardhi, ili sisimizi wale mimi, pamoja na wengineo kama watambaazi, mpaka mwili wangu wote umekuwa kidudududu na mzoga mchafu. Unyonge umekuwa rafiki yangu, na utukufu umekwenda ugeni. Aliyenipenda zaidi katika nyinyi nyote anafanya bidii kunizika, na kuniachia mimi pekee pamoja na limelotenda mwanzoni, na dhambi zangu za zamani. Hivi ninarithishwa hasara, na ninafuatwa na majuto. Na nyinyi mlikuwa mmekwisha toa ahadi kwangu mtaniwekea salama kwa maadui wabaya, lakini nyinyi hamna ulinzi wakunilindia, wala hamna nguvu kuufanya, wala nyinyi hamna ya njia. Ewe, wajamii, ninalazimishwa nijitegemee maana nyinyi mmekuja kipunjo, na mmeweka mtego kuninasia kwa udanganyifu."

Walijibu hawa, "Ewe Mfalme Msifiwe! Sisi siyo tuliyokuwapo, na wewe siyo uliyokuwa. Limelobadilisha sisi limebadilisha wewe pia, na lile limelogeuza wewe limetugeuza sisi vile vile. Usikataa toba zetu na tumia nasaha yetu." Aliwaambia," Nitaishi nanyi ingawa mtaendelea kutenda hivyo, lakini nitajifarikisha nanyi mkihalifu na vile."

Na mfalme alikalia ufalme wake, na majeshi yake yalifuata mwendo wake, na walijitihadi katika ibada. Nchi yao ilizalika , na walishinda maadui wao, na walikuza milki yao, hata akafa yule mfalme, baada ya kushika mwenendo huo huo muda wa miaka thelathini na mbili; maisha yake kwa jumla yalifika miaka sitini na minne."


Maelezo mafupi:
(1)Katika Kiingereza limetafsiriwa na neno la 'Saturn' yaani, Zuhali.
(2)Dibaji; jamdani, au nguo ya zari.

Back to TOP

II. Hadithi ya fuvu - la mfalme au la maskini?

Budasf alisema," Nimefurahi sana na hadithi hii , na ongeza sawa na ile kuzidisha furaha yangu, na rabbi nitamshukuru." Hakimu alisema :

Inasemeka kwamba kulikuwa na mfalme mwenye viongozi wa wafalme wema, aliyekuwa na majeshi waliomcha Mungu Mwenyezi, na walioabudu yeye. Na katika zamani ya baba yake, mfalme, zilitokea shida iliofumbua milki baina ya watu, na maadui walinakisi nchi zao. Lakini mtoto huyu alisukuma hawa kushikana na dini ya Mungu Mwenyezi, na kumwogopa yeye, kuomba auni naye, kujihadhari na yeye, na kukimbilia kwake. Alipotawala ufalme mwenyewe, alishinda na maadui wake, na aliungamanisha waraia wake, na alisuluhu nchi yake, na kifalme chote kilitungika kwake. Halafu, alipoona jinsi aliyekuwa alifadhilishwa na Mungu Mwenyezi, alijitaanasa, na alijivuna, na alidhulumu, hata aliacha ibada ya Mungu Mwenyezi, na alikana neema ya Mungu, na alienda kasi kuuwa wao walioabudu Mungu. Ufalme wake ulidumu na ulitawilisha hata watu wakawa wazembe hawakushika haki, waliisahau, na wakamtii yeye kufuata amri yoyote yake,hata wakafanya upesi kwenda makosani. Na kwa kuendelea hivyo, Mungu Mwenyezi hakuabudiwa, na jina lake hakutajwa baina ya watoto waliozaliwako, mpaka hawakudhani kuna Mungu ila mfalme wao. Mtoto mfalme huyu alikwisha ahadi Mungu Mwenyezi, hayati babaye mfalme, kwamba atakapotawala siku moja atakuwa mtendaji mtiifu wa Mungu Mwenyezi katika amri yake isiyofanyikwa na wafalme wo wote kabla yake, wala kuwezekana nao. Lakini, ajapomiliki, milki ilisahaulisha rai yake ya kwanza, na nia yake aliyekuwa naye; alijilevya kama sahibu za divai, na hakuweza kuamka au kuwa yu macho.

Miongoni mwa wapendwa wa mfalme kulikuwa na mtu mwema aliyechaguliwa kuwa na cheo kikuu kuliko wengineo. Yeye alisikitika sana kuona makosa yake ya dini, na usahaulifu wa lile ameloahidi Mungu. Kila aliyetaka kumwonya, alikumbuka fudhuli na jeuri yake, na hakubakia mwingine mwowote katika watu hawa ila yeye, pamoja na mmojawao mwingine aliyekuwako ukomo wa nchi ya mfalme, asiyejulikana na mahali pake wala la jina gani. Siku mmoja, aliingia ndani palipokuwa mfalme, na alikuwa naye fuvu alifichialo ndani ya nguo zake. Alipokaa kuumeni kwa mfalme, alitolea lile na akaweka mbele yake. Mara, alikanyaga juu lake, na akaendelea kulisugua mkononi mbele yake na juu ya zulia hata kikao chote kilichafuka na vyembe vilivyotokeza kwa fuvu hilo. Alipoona mfalme amelofanya yeye, alishikwa na ghadhabu kweli, na watu waliokuwa wamekaa walikaza macho kwake, hata walinzi walijiweka tayari panga zao kwa kungojea atoe amri ya kumwua yeye, lakini mfalme alitulia na ghadhabu yake. Wafalme wa zamani zile ijapoukuwa walidhulumu na walikafuru, walisaburi sana na waliwaza na kuwazua kwa kutaka hali njema ya waraia wao, na kutamani imara ya nchi zao, ili waongezee nguvu zao na kutoza ushuru kwa rahisi. Basi, mfalme hivyo aliendelea kukaa kimya mpaka yule mbele yake aliinuka na alikunja fuvu lile humo nguoni zake. Halafu, alifanya hivi hivi siku ya pili, na ya tatu vile vile.

Alipoona yeye kwamba mfalme hakumwuliza juu la fuvu lile wala hakusema lolote juu lake, aliingia na fuvu, pamoja na mizani na ardhi kidogo. Baada ya kufanya na fuvu kama alivyokuwa akifanya, alishika mizani na aliweka dirhamu katika kitanga kimoja, na ardhi ya uzito wake katika kiingine. Halafu, aliweka ardhi ile ndani ya jicho la fuvu. na alishika ukufi wa ardhi na akaiweka papo penye kinywa cha fuvu. Mfalme alipoona ameyotenda yeye, alipotea saburi yake, na akachoka mpaka kuuliza mtu yule: 'Najua kwamba umejaribu kutenda hilo kwa sababu yupo katika cheo kikubwa nami, tena umeachiwa nafasi kufanyayo hivi nami, kwa kuwa na kadiri umevyofadhiliwa na mimi. Labda unayo mradi kwa kulitenda jambo lile.'

Mtu yule alimwangukia miguu ya mfalme, na aliibusu. Alisema: ' Ewe Mfalme! Nisikilize na akili zako zote! Kwa mfano , neno ni mithali ya mshale; ukitupwa katika ardhi laini, huuthibitika, lakini ukitupwapo maweni, haushikwi. Tena, mithali ya mshale ni kama mithali ya mvua; ukipiga juu ya ardhi njema imeyopandwa, yaanza kuota, lakini ukipata bwawa-chumvi, haikuwi. Maana, hawa za watu ziko mbali-mbali, na akili na hawa hushindana mieleka katika roho. Hawa ikishinda akili, mtu huwa na harara na ujinga, lakini kama hawa imeshindwa , katika mambo yake mtu yule hawezi kukoseka. Na mimi tangu ujana nilikuwa nikapenda elimu sana na nilikuwa na tamaa ya kujifunza, na niliipenda zaidi kuliko mambo yote mengine. Na sikuiacha kujifunza kamwe ila kufikia cheo cha elimu kikuu. Sasa, siku moja, nilipokuwa nikatembea makaburini, nilipata kuona fuvu hilo lililotokeza kwenye makaburi ya wafalme. Nilichukiza na mahali palipokaa lile, na kutengwa na mwili wake hivyo niliona uchungu kwa ajili ya wafalme hao. Basi, nilikumbatia nalo, na nilichukua lile nyumbani yangu. Nililovika na dibaji na kunyunyishalo na maji ya waridi, na nililowekea juu ya zulia. Nilisema, ingawa hilo ndilo mmojalo la mafuvu mengineyo ya wafalme, kutukuzwa na mimi hatakuwa ya bure, na hivyo litarudishwa tena katika jamala na fahari zake. Lakini, ingawa ni mmojalo la mafuvu ya maskini, kukirimu hilo hatakuwa na maana hata kidogo. Niliendelea kufanya hivi kwa muda wa siku chache, na sikuwaza badiliko lolote katika sura yake. Nilipoona hilo, nilimwita mtumishi, na yeye alikuwa mnyonge kuliko watumishi wote wangu, kulidharau lile, lakini hali lake lilikuwa lili hili, kwa kulitukuza au kulidharau. Nilipoona hilo, nilikwenda kwa mahakimu na nikawauliza hao, lakini sikupata mwelezo wake kwao. Halafu, niliwaza kwamba mfalme ni upeo wa elimu na ukaji wa upole. Kwa hivyo, nilikuja kwako kuwa na hofu binafsi, ambayo sikuweza kukuomba chochote ingawa hungeniambia kuanza kwanza. Sasa, nataka uniambie, ewe Mfalme, hilo fuvu la mfalme au fuvu la maskini? Na nilipovia baadaye na shauri lake, nilifikiri jambo la jicho lake ambalo halikujawa lolote hata ikawa halikutosheka lo lote liliopo chini ya mbingu, na likaangaza kupatia lile juu ya samawati. Na mara nilikwenda kufikiria nini yaweza kuziba hilo, na uzito wa ardhi wa dirhamu moja ilitosha kulijazia na kuliziba. Tena, nilitazama juu ya kinywaji chake ambacho hakikupata kujawa na chochote, na kilijazwa sasa na ukufi wa ardhi. Ewe mfalme, kama utaniambia hilo ni fuvu la maskini nitakuhoji nimelookota katikati ya makaburi ya wafalme. Halafu, nitasanya mafuvu ya wafalme pamoja na mafuvu ya maskini, na ikiwa mafuvu yenu huonyesha fadhili kuliko hilo, itakuwa kama umeyosema. Lakini, ukiniambia fuvu ndilo ni mmojawayo la wafalme nitakueleza mfalme huyu aliyekuwa mwana fuvu na alikuwa amekwisha pata na fahari ya kifalme, na uzuri wake, kama wewe katika ufalme wako sasa. Hasha , ewe mfalme, ufike hali ya fuvu hilo, na kukanyagwa na miguu mpaka kuchanganyikwa na matifu, tena, kuliwa na madudu, na kupata baada ya wingi, uchache, na baada ya heshima, unyonge. Kishimo cha dhiraa nne kitakufaa kwako, kifalme chako kitarithiwa, habari zako zitaisha, vyote umevyojenga vitaharibika. Walioheshimu wewe watakubeza, na waliodharau wewe watakutukuza. Heri itakuwa na maadui wako, na wao walikusaidia watatwezwa , na uvumbi utakutengesha na dunia. Tukapokuita, wewe hutasikia, na tukikutukuza, wewe hutapokea, na tukikudharau wewe hutakasirika. Watoto wako watakuwa yatimu, na wanawake wako wajane, na ahali zako watafanya bidii kuposana na waume wengine.

Aliposikia hii, moyo wake ulifadhaika na macho yake yalibubujika machozi, tena alilia na alitoa sauti kiliolio. Mara mtu yule kwa kuona vile akafahamu manaeno yake yalikuwa yamekaza ndani ya mfalme na maneno yenyewe yalimathiri kweli. Alijipa moyo kwake kukariri tena amevyosema.. Mfalme alisema kwake, " Naomba Mungu akupatie zawadi za njema, na apatie hawa watu ambao waadhimu kwangu, zawadi za ovu. Naapa kwa aushi yangu, nimeelewa maana ya haya makauli yako, na wewe umewaza jambo langu. Watu walipata habari zake na wote waliostahilika walielekea naye, kumhitimisha kwake na heri, na aliendelea hivyo mpaka alifariki dunia.

Back to TOP

III. Mwanamfalme mvulana aliyetoroka nyumba yake , na alikataa kuowa Mwanamfalme msichana

Halafu, mtoto wa mfalme akasema: "Nisimulie tena methali nyingine."

Hakimu alisema, Wasema awali ya zamani kulikuwa na mfalme aliyetamaa sana kupata mzao, na hakuwa kutojaribu zote za madawa zinayotumikwa na watu ila zililetewa na kufanyikwa. Baada ya muda tawili katika jambo hilo, mmojao wa wake zake alishika mimba, na akazaa mtoto wa kiume. Alipokua na kulelewa, alichukua hatua siku moja na akanena: "Jihadhari, mtakuwa wepesi." Akachukua hatua tena na akasema: " Mtaoza." Baada ya hatua ya tatu, alisema: "Halafu, mtakufa." Mara akarejea kutenda vitendo vya watoto. Mfalme akawaita waalimu na manajimu na akasema, "Niambieni shauri la mtoto wangu huyu". Walitazamia mambo yake na shauri lake, lakini walikosekana na yeye, na hawakuwa na elimu katika jambo lile. Mfalme akapoona hawakuwa na elimu juu jambo hilo, akampeleka yeye kwa mama wa kunyonya, na wakaanza kumlea, ila najimu mmoja aliyesema, "Atakuwa mwongozi wa dini". Aliweka walinzi kumtenga yeye na yeye alipevuka hata alikuwa kijana., na aliondoka kwa aya na mlinzi waliyekuwa naye na alienda sokoni. Kwa kuangalia tu, akaona maziko na akasema, " Nini hiyo? " Walijibu, " Mtu amekufa " Aliuliza," Alifiwa kwa nini?" Walisema, " Alikuwa mzee na siku zake zilikwisha na alipatikana na ajali , na akafa". Aliuliza, " Kwani alikuwa na siha, yu hai, na alikuwa akitembea, na akila?". Walisema, "Naam". Aliendelea na mara akamwona mzee mkuu. Alisimama kumwangalia yeye kwa ajabu mno. Alisema, "Nini hiyo?" Walimwambia, " Ni mzee mkuu, jana lake limekwisha na amekuwa mwenye mvi". "Kwani alikuwa sahihi kabla ya kukonga?" Walijibu, " Naam". Baadaye, aliendelea na mara akamwona mgonjwa amelala chali. Alisimama kwa kuona ajabu na aliwauliza, ""Nini hiyo?" Walisema, " Ni mtu mgonjwa". Alisema, " Na alikuwa na siha kabla alishikwa na maradhi? " Walijibu, " Naam." Alisema, " Wallahi, kama mnasadikika watu lazima ni wajinga." Kijana walimpotea baadaye, na alitafutiwa, kumbe alikuwa sokoni. Wakaja wakamchukua , na walienda naye na waliingiza nyumbani kwake. Alipoingia ndani ya nyumba, alijitupia mgongoni wake na akatangaza macho juu ya paa la mti wa nyumba na alisema: " Hili ilikuwa nini?". Walisema: "Lilikuwa jiti liliota na lilikuza na miti yake. Halafu, lilikatwa, na nyumba hiyo ilijengwa, na miti hii ilipangwa juu yake."

Na wakati alikuwa katika mazungumzo yake, mfalme alipeleka habari kwa waangalizi wake akasema," Mtazameni, je amesema au kunena lolote?" Walisema, "Naam, amesema maneno tuliyodhani kama wasiwasi tu." Alipoona hivyo, na baada ya kusikia yote mtoto wake aliyasema , aliwaita waalimu na akashauriana nao lakini hakupata kwao ufahamu wake ila mtu wa kwanza, lakini hakukubali na maneno yake. Halafu, mmojawao akasema," Ewe mfalme! Ungalimwozea, vyote vyake unavyoona vitatoka, na atajifahamu, na atapata akili na busara." Mara mfalme alituma watu kote nchini kumtafutia na aliposwa na mwanamke mmoja mzuri wa kupendezwa kuliko wote, na waliozesha naye. Walipoanza lima ya arusi(1), wachezaji walicheza, na mazumari walipiga zomari. Mvulana yule aliposikia milio yao na sauti zao, alisema, " Nini hiyo?" Walisema, "Hao ni wachezaji na mazumari wameokutana kwa arusi yako." Mvulana alisukutu. Baadaye, ilipokwisha walima na watu walichwewa, mfalme alimwita mwanamke wa mtoto wake na alisema kwake, " Sina mtoto mwingine ila mvulana huyu. Sasa, ukaingia kwake, uwe na latifu, na nenda karibu naye na uonyeshe upole." Basi, mwanamke alipoingia kwake, alijaribu kusogea karibu na kumjongelea alipo. Mvulana alisema, " Pole pole! Kuna usiku kucha, Mungu akuwekee, subiri hata tumekula na tumekunywa." Aliagiza chakula na alianza kula . Alipomaliza, mwanamke alianza kunywa, na mara sharabu ikimlevya alilala usingizi.

Mvulana alisimama na aliacha chumbani kwake, aliepuka walinzi na mabawabu kisirisiri mpaka alijiondoa nje. Halafu, alienda matembezi mjini , na kule alimkuta kijana mwingine mkazi wa mji ule, na alimfuata yeye. Tena, alimtupia nguo alikuwa amezovaa yeye, na alivaa nguo nyingine zake, na alifanya juhudi mno kutoarifiwa. Wote wawili walitoka mjini na waliendelea usiku kucha hata, karibu asubuhi, waliogopa wasitafutiwe na walisimama. Kuwa asubuhi, wajakazi walifika kule na wakamkuta yeye amelala. Walimwuliza, " Mume wako ni wapi ?" Alisema, " Sasa hivi alikuwa hapa na mimi ." Walitafuta mvulana lakini hawakuvumbulia yeye. Na mvulana na mwenzake, ilipochwewa, walianza safari tena, wakiendelea usiku kuchwa na wakajifichia kwa siku, mpaka walipata kufika nchi ya Sultani mwingine.

Mfalme huyu milki yake ambapo walifikia hawa alikuwa na binti aliyekuwa amepatana naye kuwa asiozeshe ila pamoja na mwingine anayempendezwa naye na amemridhisha. Tena, alikuwa amejenga chumba kilichokuwa juu mbinguni, na kiliangalia chini kwa njia. Na yeye alikuwa akikaa pale kutazamia wote waliopita , kwenda na kurudi. Na wakati alipofanya hivyo, alimwona mvulana yule anatembea sokoni pamoja na rafiki yake, na mavazi yake machakavu. Mara alipeleka habari kwa baba yake, " Nimekwisha penda mtu. Ungaliozesha mimi na mtu ye yote , tafadhali niozeshe naye." Hata , alifikiwa mama ya msichana na akaambiwa, "Binti yako amekwisha penda mtu, na amesema hivi na hivi." Na yeye alikwenda kwake, amejaa na furaha , apate kumwona mvulana na hao walimwonesha yeye. Mama yake alitelemka mpaka aliingia palipo kuwa mfalme, na alisema, "Angalia, binti yako amempenda mvulana." Mfalme alikubali kuenda kwake kumwona. Baadaye alisema, "Nimwonyeshe." Walimwonyesha yule kwa mbali." Yeye aliamuru wavalisheni nguo nzuri, na alitelemka kumsaili na kuzungumza naye. Alimwuliza, "Wewe nani, na umetoka wapi?" Mvulana alisema, "Kwa nini unanisaili hivyo? Mimi ni mmojawao maskini tu" Na yeye alisema, " Wewe ni mgeni, rangi yako haifanani hata kidogo na wakaazi mjini." Mvulana alisema, " Mimi siyo mgeni!" Mfalme alimhojihoji sana asadikie yeye na kisa chake, lakini alikataa. Kwa kuwa hivyo, mfalme aliamuru watu wamlinde na waangalie anakwenda wapi, lakini yeye asijue. Mfalme alirudi kwa ahili zake na aliwaambia, " Nimemwona mtu aliyekuwa kama mtoto wa mfalme, lakini yeye kasema hana haja ya ile mmeyoshawishi moyoni." Halafu, alituma mtu kwake kumwambia yeye," Mfalme anakuita" Mvulana alisema," Mbona mfalme ananiita, na mimi sina haja naye, na yeye hajui mimi nani?" Hata pamoja na kirihi yake, alichukuliwa mpaka palipokuwa mfalme. Aliamuru kiti kiletewe, na kilipowekwa , aliketiwa juu ya kile. Mfalme aliwaita mwanamke wake na binti yake, na aliketia hao wawili nyuma ya kiwambo. Baadaye, mfalme alisema kwake, " Nimekuita hapa na nia nzuri. Mimi ninayo msichana anakupenda sana, na ningependa wewe kukufunga ndoa naye. Na kama wewe ni maskini, nitakufanya mtu wa mali, na nitakupanza daraja na nitakutakarimu." Mvulan alisema, " Sina haja ya makusudio haya. Lakini, ungependa, ewe mfalme, nitakuhadithia methali. " Alisema, "Ndiyo, bila shaka."

Mvulana alianza : "Wasema mfalme mmoja alikuwa na mwana, na kijana huyu alikuwa na marafiki waliopika chakula na walimwalika yeye. Alikwenda kwao, na wakala na wakanywa mpaka wakalewa, na wakalala usingizi. Usiku wa manane, mwanamfalme aliamka na alikumbuka wajamaa wake. Basi, aliondoka kurudi nyumbani kwake bila kuamsha yo yote mwingine. Alipokuwa njiani tu mara alishikwa na ulevi, na alipoona kaburi njiani alidhani ni mahali pake. Aliingia ndani lenye nuko la mauti na alifikiri lile zuri kwa sababu ya ulevi wake. Na kaburini palikuwa na mifupa aliyehesabu kuwa kitanda kimechotandikwa chake, na mwili uliofariki hivi hivi karibuni na uliokuwa umevunda alidhani kuwa bibi yake. Alikaa karibu naye, na alimfumbata , na alimbusu, na alicheza naye usiku kuchwa. Kwa kupata na fahamu, alifahamu, na kukuwa na macho, aliona kumbe alikuwa amelala juu ya mwili maiti ulionuka uvundo, na uliochafusha nguo zake na mwili wake, na aliangalia pale kaburini penye mafu yaliyokuwamo ndani, na alienda zake. Ubaya uliokuwa umeambata naye alitaka kujifichia na macho ya watu wasiangalie kwake alipokwenda kuelekea mlango wa mjini. Aliukuta wazi, na aliingia ndani mpaka alifika ahilini , na alishukuru kutokutana na yo yote awezaye kumjua na yeye. Halafu, alivua nguo zake alizokuwa amevaa, na aliosha na alivaa nguo nyingine na alitia manukato. Mungu akuwekee umri wako, ewe mfalme! Wafikiri huyu angependa kurejea binafsi kwa kile kilikuwako?" Mfalme alijibu, "La!" Mvulana alisema, " Na mimi yeye!"

Mfalme alielekea na mwanamke na binti yake na alisema, " Nimekwisha eleza nyinyi wawili yeye hataki kufanya kile mnachotaka afanye." Mama yake alisema, "Ewe mfalme, ni wewe ndiyo umekosa kueleza na kusifia binti yangu, lakini mimi nitakuja nje na nitazungumza naye." Mfalme aliuliza mvulana, " Mke wangu anataka kuzungumza na wewe, na kutoka nje kwako, isipokuwa hakutoka kabla hivi kumkuta mwingine yo yote." Mvulana alisema, "Haya, mwambie aaje nje angalipenda hivyo." Basi, alitoka nje na alikaa kitako, na alisema kwa mvulana," Njoo mwenye riziki na uzuri zimekupewa na Mungu na nitakuozesha na binti yangu. Ungekumwona kadiri Mungu Mwenyezi amepewa yeye jamala na urembo, ungefurahisha mno." Mvulana alitazama mfalme, na alisema, " Eti, siwezi kukusimulia methali?" Alijibu, "Ndiyo!"

Alisema, "Wezi waliagana watakuingia hazina ya mfalme kuiba, na walitoboa ukuta wa hazina na waliingia ndani. Pale, waliona jinsi ya vitu havikuona mbele abadan,na walipata na kulla(2) ya dhahabu iliyotiwa na muhuri ya dhahabu. Walisema," Hatutaona tena kitu kingine kizuri kuliko kulla hii, ya dhahabu, ambayo imeyofungwa na dhahabu, na vile vimo ndani yake vitakuwa vizuri zaidi kuliko vyote tumevyoona." Waliichukua na walienda naye mpaka walifika kichaka, kila mmojawao asiweze kuamini mwingine naye. Kule, waliifunua, kumbe kulikuwamo nyoka walioruka nyusoni zao, na waliuwa wote pamoja. Ewe mfalme, Mungu akuwekee umri wako, kwani wafikiri yo yote akijua na iliyofanyikwa na iliyotokana na kulla hii aweza kurudisha mtazamo wake juu ya ile tena?" Alijibu, "Hapana!" Alisema yeye, "Ati na mimi yeye!"

Sasa, msichana alisema kwa baba yake," Nipe ruhusa mimi niende mwenyewe kwake kuzungumza naye. Akinadhari mimi na jamala yangu, urembo wangu, uzuri wangu, na umbo wangu na vile nimevyopewa na Mungu Mwenyezi ya jamala, hatawezi kutonipendea." Mfalme alimwuliza mvulana, " Je, binti yangu anataka kutoka nje kwako, na mpaka sasa hajatoka kwa yo yote mwingine abadan." Alijibu, " Acha atoke angependavyo!" Basi, alitoka nje kwake na kweli alikuwa na sura nzuri kuliko zote za watu. Alisema kwa mvulana, "Kwani umemwona mwingine namna yangu abadan, au aliyekuwa na timamu zaidi, au na jamala zaidi, au na ukamilifu zaidi, au na uzuri zaidi? Na mimi nimekwisha penda na wewe, na kukustahabu." Mvulana alitazama kwa mfalme na alisema,"Eti, siwezi kukusimulia methali?" Yeye alisema, "Ndiyo, bila shaka."

Mvulana alisema," Ewe mfalme, wanadai kwamba mfalme alikuwa na watoto wawili, na mmojawao alinyang'anywa na mfalme mwingine. Alifungwa mahabusini, na aliamuru wo wote wapitao wasiende bila kumtupia na jiwe. Aliishi hivi kwa muda. Halafu, ndugu yake alisema na babaye, "Nipe idhini niende kwa ndugu yangu ili kumkomboa yeye na kutumia maarifa kumwokoa. " Alisema, " Nenda, na chukua na wewe vyote utakavyo vya mali, na bidhaa na wanyama wa kupanda." Basi, alifunga safari (3) pamoja na vifaa, na alichukua naye wanawake waimbaji na waliaji. Walipokaribia mji wa mfalme yule , mfalme alipata kujua anakuja, na aliamuru watu wote waende kumkutana naye na wote walitoka. Tena, aliamuru akae katika nyumba nje ya mji, na mvulana alishuka kukaa nyumbani ile. Alipokalisha nyumba, aliandaa bidhaa zake, na aliwaambia vijana wake waziuzie watu na kusahilisha ununuzi wao, na kuonyesha upaji kwao. Hao walifanya hivi. Alipoona watu wameshughulika sana na biashara, aliondoka na aliingia mjini. Alikuwa amekwisha fahamu mahali pa kufungwa ndugu yake, na alipofika pale kifungoni, alichukua jiwe na alilotupia kutazama nini imeyobakia nafsi ya ndugu yake. Yeye alilia kwa siaha alipopigwa na jiwe, na alisema, " Umeniuwa! " Mlinzi alishtuka na hii, na alikwenda kwake na alimwuliza,"Umelia kwa nini? Umetokalo na jambo gani ? Hatujapata kukusikia neno lolote kwako na sisi tumekuadhibisha wewe kwa muda mrefu sana, na umegongwa, na wote wameopita hapa wamepiga wewe na jiwe. Sasa mtu huyu amepiga wewe na jiwe, mbona umelia hivyo kwa siaha?" Alisema yeye, " Watu wengine walikuwa wajahili juu ya mambo yangu. Huyu amenitupia jiwe na ujuzi." Baadaye, ndugu yake alirudi nyumbani yake, palipokuwa na mali yake, na alisema kwa watu, " Ikiwa kesho, rudini kwangu na nitawakunjushia mavazi mazuri na bidhaa ambazo hamjakuona mifano yake kabla hiyo." Basi, walikwenda zao siku ile, na kucha siku ya pili wote walirudi pamoja kwake. Yeye aliagiza nguo na alizikunjua, na aliamuru waimbaji na waliaji na aina nyinginezo zote nazo za kushawishia watu, na walianza mambo yao na wote wakashughulika. Mara alikwenda kwa ndugu yake, na alikata mapingu yake. Alisema, "Nitakuuguza." Alimnyang'anya kwa siri na alimchukulia kutoka nje ya mji. Alipaka majeraha yake na dawa aliyekuwa naye mpaka, alipoona raha, alimsimamia njiani na alisema, "Nenda hata uone safina itakuwa imetayarishwa kukusafirisha baharini." Aliendelea mwenendoni na mara alianguka shimoni mwenye tinini(4). Juu ya shimo palikuwa na mti thabiti. Alitazamia mti ule. Kumbe, palikuwa vizimwi kumi na mbili kileleni cha mti, na chini wake, panga kumi na mbili. Panga hizo zilikuwa zimefutwa na zikuangika. Hakuishi kujistahimili na kuvumbua mpaka alikamata tawi la mti na kwa kuning'inia nalo alijiokoa. Aliendelea mpaka alifika baharini na aliiona safina kando ya pwani iliyokuwa imetayarishwa kwenda na yeye. Alirakibu juu yake na alisafiri mpaka ilimfikisha yeye kwa ahali zake. Ewe Mfalme, Mungu akuwekee umri wako, wadhani yeye aweza kurudi tena kwa vile alivyoona, na alivyokuta? Alisema, "Hapana!" Yeye alisema, "Ati na mimi yeye!"

Basi, walikata tamaa naye. Lakini, yule kijana aliyesuhubiana naye kutoka mji wake alikuja na alimnong'oneza, alisema, " Kumbusha mimi kwake na niozeshe na yeye." Mvulana alisema kwa mfame, " Ati, huyu anasema ningependa mfalme tafadhali afanye kuniozesha na mtoto wake." Mfalme alijibu, " Nitakufanyia." Baadaye, alisema kwake, "Eti, siwezi kukusimulia methali?" Alisema, " Ndiyo, bila shaka."

Alisema, "Kulikuwa na mtu aliyeishi pamoja na wajamaa wake, na aliyepanda meli na alipita bahari masikuni. Halafu, safina yao ilivunjika karibu na kisiwa cha bahari kilichokaliwa na gilani(5). Wote walitota ndani ya maji ila yeye. Bahari ilimtupa yeye kisiwani, ambapo gilani palikuwa na macho ya kuangalia juu ya bahari.. Gula mmoja alikuja na alimpenda yeye na yeye alimwoa. Ilipokuwa asubuhi, alimwua yeye na alichangua viungo vyake kuvigawanya mwenye sahibu zake. Vivyo hivyo vilifanyikwa na mtu mwingine, aliyechukuliwa na mtoto wa kike wa mfalme wa gilani, na aliyeenda naye, na alilala naye na alifunga nikaha naye. Sasa, mtu huyu alijua lote lililotukia na yule aliyetangulia yeye mwenyewe, na hakulala hadharini, hata ikifika asubuhi,na akiamka gula, yeye akajiondoa mpaka alifika pwani. Kumbe, kule palikuwa na safina. Aliwaita kwa sauti wajamaa waliyomo, na aliwaomba wamsaidie. Walimpakiza yeye hata walijilia na ahali zake. Gilani waliamka asubuhi, na walienda kwa gula aliyekuwa naye, na walisema kwake, " Wapi mtu aliyelala usiku na wewe ?" Yeye alisema, "Ametoroka kwangu." Hawa walimwita yeye mwongo, na walisema," Wewe umemkula yeye , ili kujitwalia yeye peke yako na kutoshirikiana na sisi. Usingetuletea na yeye, tutakuua." Basi, alipita juu ya maji mpaka alifika nyumbani yake na pakuishi yeye. Aliingia ndani na alikaa naye, na alisema kwake, "Umekuta nini katika safari yako hii?" Alisema," Nimezikuta balaa tu, na Mungu ndiye ameniokoa nazo," na alimmsimulia kisa chote. Yeye alisema, " Na umeokolewa kweli?" Alisema, " Naam." Aliendelea, na yeye alisema, " Na mimi ni gula, nimekuja kukuchukua." Alisema, "Nakuomba na Mungu usinifishe. Mimi nitakuletes kiongozi mwingine badala yangu." Yeye alisema, "Hivi nitakurehemia." Walienda pamoja mpaka waliingia hadhara ya mfalme." Yeye alisema, " Sikilize sisi wawili, Mfalme Msuluhishi wa Mungu. Mimi nilifunga ndoa na mtu huyu, na nilimpenda yeye zaidi kuliko wote wengine. Halafu, yeye alichukia na mimi, na alikirihi kusuhubiana na mimi. Sasa, kagua shauri letu." Lakini, mfalme alipomwona yeye, aliajabika na jamala yake, na alijitenga pamoja na mtu yule na alinong'ona kwa siri naye. Alisema kwake, " Mimi ningependa wewe kumwachia yeye , na mimi nitakumwoa yeye." Alisema, " Naam, Mfalme Msuluhishi wa Mungu. Hamfai yeye mwingine ila na mfalme." Basi, mfalme alifunga ndoa naye, na alilala usiku pamoja na yeye, hata ilipokuwa alfajiri alimchinja, na alikata viungo vyake, na alivichukua kwa marafiki wake. Ewe Mfalme, wadhani yo yote anapojua hayo yote aweza baadaye nenda kurudi tena kwayo? Alisema yeye, " Hapana!"

Halafu, yule mchumba mwanaume alisema kwa mvulana, " Siwezi kufarikia na wewe, tena sioni haja na ile iliokuwa mradi wangu." Waliondoka pale palipokuwa mfalme, na sote wawili waliabudu Mungu Mwenye enzi na jalali, na walitembea mbali nchini. Na Mungu Mwenye enzi na jalali aliwaongoza watu wengi kwa sababu ya hao wawili. Shauri la mvulana lilifika ukuu , na jambo lake liliongezwa mpaka upeo wa nchi mbali. Baadaye, alikumbuka baba yake, na alisema, "Laiti ningekumpelekea mtu kumwokoa yeye humo aliokuwamo." Basi, alipeleka na mtumwaji alipofika kwake akasema, " Mtoto wako anatoa salamu", na alimpa kisa cha habari zake, na mambo yake. Na babaye, pamoja na ahali zake, walienda kwake, na yeye alifaulu kuwaopoa wenye waliokuwamo.


Maelezo mafupi:
1.lima ya arusi; wali wa lima = walimah ( wedding feast )
2.kulla; sanduku ndogo au chungu
3.rahilah (rawahil); ?ngamia kike; shadda rahilatahu = funga safari
4.tinini; mnyama wa bahari hasa ya hadithi ya zamani siyo ya kawaida , pengine ni kama joka lenye mabawa, magamba, na miguu minne yenye kucha. yaani Drako.
5.gula, mengi, gilani; aina ya pepo kiarabu, kwa kawaida, kike kibaya, huleta msiba mkubwa.

Hadithi hizi zilitafsiriwa kumbuko ya mama mzee yangu aliyefariki dunia baada ya miaka zaidi ya mia mmoja


Back to TOP

I Previous page I Full page List I Next page

© M. E. Kudrati, 2006:This document may be reproduced and redistributed, but only in its entirety and with full acknowledgement of its source and authorship