Raphaeli - New famous Chagga rap!

Ni namna gani ah, ni jinsi gani tutawini  maishani
mpaka siku tunasema buriani, ah x3

Ilikuwa Jumapili nkamuona Raphaeli, amekaa juu ya
nini, ni juu ya baiskeli,
namuuliza anaenda wapi kaniambia anaenda feri,

Huko feri ni kwa nani, kwa lile jitu tapeli,
sasa utamuona wapi, atakuwa kwenye meli,

kwenye meli ndo wapi, ndo  huko huko feli

Baadaye  namuona huyo huyo Raphaeli

 anacheza na nani,na yule dada Mary,
namuuliza  Raphaeli hapa ndiyo feri,

anasema siyo hivyo,mwenziyo unajua nimeharibikiwa  na ile baiskeli, nategemea kwenda kule Oysterbay,

nako huko ntamkuta brother  Mtei,
yeye ndiyo atakayenipunguzia bei ya spea za  baiskeli

Ah, Ni namna gani ah, ni  jinsi gani tutawini maishani
mpaka siku tunasema buriani, ah x3

Kesho yake nikatoka moja kwa moja kwa Raphaeli,
nikamkuta nyumbani anasikiliza CD ya R. Kelly,

 nkamuuliza Raphaeli unayo CD ya Makafeli,
akaniambia na Makafeli, R. Kelly na Mariah Carey
Sisi hatukukaa,

Tukatoka moja  kwa moja haooo, mpaka kwenye baa
unaambiwa watu walikuwa wamejaa,

Kengeleki zimeshikamanan,baiskeli na motocar,

Basi tukaagiza masanga pale  na kiti moto tukaanza
kupata moja baridi moja moto
wakati tunaendelea eeeh,

kidogo tu huyooo katokea mzee Urassa

na ile  Land Cruiser yake new model ya kisasa power engine 2.4,
filling system ya kisasa,
unaambiwa ni automatic kuanzia viti hadi  vitasa
Basi alikuwa na laki tatu mfukoni, akajishika  kiunoni

akatuangalia usoni,
akatudharau akaingiza mkono mfukoni

akatoa pesa akaweka pale mezani kisha akaenda chooni

Sisi  basi tukaanza kulewa, tukalewa tukalewa, yesu
wangu,
tulilewa tulilewa tulilewa tulilewa, wakaongezeka ndugu zetu kutoka
sehemu mbalimbali za kilimanjare, Marangu, Machame, Uru, Kishmoto, Kibosho,Mwika, Mbunju mpaka Kiborloni,

unaambiwa Tarakea mpaka huku sehemu za Rombo,
wote pale wakawa wamemiminika,

 Masawe alikuwepo, Mariale alikuwepo,Shirima alikuwepo, Mangi
alikuwepo, Mrema alikuwepo, Ndosi alikuwepo, Mlei alikuwepo, Asei
alikuwepo,mama Prisca alikuwepo, mama Manka alikuwepo,  Minja
alikuwepo, Kiluwa alikuwepo, na huyo mtoto anakaa mtaa wa pili nani?
Chuwa,eti Chuwa naye alikuwepo

Ni namna gani  ah, ni jinsi gani tutawini maishani
mpaka
siku tunasema
buriani, ah  x3

Wakati tunaendelea kupata  pale masanga na kiti moto,
Raphaeli na Masawe haooo, wakatoka
sikujua kinachoendelea, nikajua wanaenda kuruka majoka
kwa sababu  kulikuwa na mziki wa Reggae, charanga na ule mziki wa  kufokafoka.

Akilini mwangu nilikuwa nafikiri kwamba mambo yataenda  yakifanya
nini,yakienda yakinyooka.
Kumbe huko walikokwenda   walienda kuwachokoza wake za watu wakawa wameketi,

wakaanza kuwashikashika  mabegani mpaka zile sehemu zao nyeti.

Basi waumbe zao nikawaona  wamechukia

maneno machafu wakaanza kuwatupia,

 Kinabo wewe,wacha mke wangu  kima wewe unamshikia nini huko, mara
huyu kamtukana mwezake
sijui kamwambia  fala wewe, huyu kamrudishia maneno yale na lile,

 basi tu
ikawa vurugu  mechi.

Basi wale wanaume nikawaona  wamebeba mawe

wakataka wamponde nayo Masawe.
Basi Raphaeli akamrukia teke  mmoja wao akamuangusha palepale.

Akataka akimbie hajafika mbali akakamatawa na nani, na yule
afande Charle,

Asa mie nikamuambia afande  Charle, naomba basi umruhusu huyu
Raphaeli nyumbani akalale.

Akaniambia ni lazima kituoni huyu Raphaeli leo akalale,

Sasa nikaona  sina tena la kufanya,

Raphaeli ndo huyo tena amesha ulowanya.
Kwanza mimi kichwani lager zishanchanganya ikabidi  tungoje
kesho tu tujue ni kitu gani tutafanya.

Basi kama Raphaeli ndo  kama ameua,
basi pesa zangu zote polisi watakuwa wamechukua,

 

yesu wangu, yelleeuwiii

Pesa ni maua maana maua  hunyauka, vile vile huchanua

Ah, Ni namna  gani ah, ni jinsi gani tutawini maishani

mpaka siku tunasema
buriani, ah  x3