Bismillahir Rahmaanir Rahim

MUHTASARI WA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU KWA MADRASA NA SHULE ZA MSINGI

DARASA LA V
FANI MADA MADA NDOGO LENGO (MWANAFUNZI) MBINU ZA KUFUNDISHIA VIFAA/REJEA
QUR'AN Kusoma, kuhifadhi na kutoa ujumbe. Kuhifadhi na tafsiri ya sura zifuatazo: -
 • Nuhu hadi At-Talaq.
 • Tafsiri na ujumbe wa albayyina hadi Al-A-alaa
Ahifadhi na kutafsiri Qur-an na apate ujumbe uliomo na aweze kuufuata.
 • Mwalimu asome kila sura huku wanafunzi wakimfuatisha, kisha wanafunzi waandike sura hizo na kuzihifadhi.
 • Atoe tafsiri na ujumbe wa kila sura na kuwapata wanafunzi mazoezi ya kutafsiri na kubainisha ujumbe. Kisha aandike ubaoni tafsiri ya kila sura na jumbe wake na wanafunzi wanakili madaftarini mwao.
Kitabu cha V (IPC)
TAWHIID Kuamini Malaika wa Allah (S. W.).
 • Umuhimu wa kuamini Malaika.
 • Sifa za Malaika.
 • Kazi za Malaika.
 • Maana ya kuamini Malaika katika maisha ya kila siku.
Aweze kueleza athari ya kuamini Malaika katika maisha ya kila siku, Sifa na kazi za Malaika.
 • Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa maelezo na kuandika ubaoni umuhimu wa kuamini Malaika katika Uislamu, sifa na kazi za Malaika.
 • Aonyeshe na kusisitiza ni vipi imani ya kweli juu ya Malaika itakavyomuathiri muumini katika maisha ya kila siku.
Kitabu cha V (IPC)
Kuamini Vitabu vya Allah (S. W.)
 • Umuhimu wa kuamini vitabu.
 • Vitabu vya Allah vilivyotajwa katika Qur-an.
 • Tofauti ya Qur-an na vitabu vingine.
 • Uthibitisho kuwa Qur-an haitabadilishwa na waharibifu.
 • Maana ya kuamini Vitabu vya Allah (S. W.)
Atambue maana ya kuamini Vitabu vya Allah (S. W.) katika maisha ya kila siku.
 • Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa maelezo na kuandika ubaoni umuhimu wa kuamini vitabu, vitabu vya Allah (S. W.) vilivyotajwa katika Qur-an, tofauti ya Qur-an na vitabu vingine, uthibitisho kuwa Qur-an haiwezi kubadilishwa na mwanaadamu.
 • Asisitize mwenendo anaotakiwa awe nao muumini wa kweli wa vitabu vya Allah (S. W.)
Kitabu cha V (IPC)
FIQ-H Uislamu
 • Maana ya Uislamu.
 • Nani Muislamu.
Aweze kumtambua Muislamu wa kweli. Mwalimu aeleze maana ya Uislamu na kutokana na maana hiyo abainishe ni yupi hasa ni Muislamu wa kweli. Kitabu cha V (IPC)
Swala
 • Kusimamisha Swala.
 • Umuhimu wa kusimamisha Swala
 • Lengo la Swala
Aweze kufahamu umuhimu wa Swala katika maisha ya kila siku na aweze kuswali kulingana na lengo la Swala.
 • Mwalimu aonyeshe tofauti ya kuswali na kusimamisha Swala.
 • Kwa kutumia Qur-an na Hadithi mwalimu awafahamishe wanafunzi umuhimu wa Swala na lengo lake.
 • Pia awafahamishe wanafunzi faida mbalimbali zinazopatikana kwa mwenye kusimamisha Swala.
 • Aonyeshe ni vipi lengo la Swala litafikiwa na mwenye kuswali.
Kitabu cha V (IPC)
Zakat
 • Umuhimu wa Zakat na Sadaqa.
 • Masharti ya utoaji zakat na Sadaqa.
 • Lengo la Zakat
Atambue umuhimu wa utoaji mali katika jamii ya Kiislamu.
 • Kwa kutumia Qur-an na Hadithi, Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa kueleza na kuandika ubaoni juu ya umuhimu na masharti ya utoaji wa zakat na sadaka.
 • Awafahamishe lengo la Zakat na jinsi linavyofikiwa.
Kitabu cha V (IPC)
Funga ya Ramadhani.
 • Lengo la funga.
 • Tarawehe, Lailatul-Qadri na Itiqaf.
 • Zakatul-Fitri.
 • Idil-Fitri.
Aweze kufikia lengo la funga. Kwa kutumia Qur-an na Hadithi, Mwalimu aeleze na kuandika ubaoni juu ya lengo la swaumu na linavyofikiwa, Swala ya Tarawehe, Lailatul-Qadri. Kitabu cha V (IPC)
Funga za Sunnah.
 • Funga zote za Sunnah.
 • Umuhimu wa funga za Sunnah.
Atambue umuhimu wa funga za Sunnah na aweze kuzifunga.
 • Mwalimu abainishe funga zote za Sunnah kwa kurejea Hadith.
 • Aonyeshe umuhimu wa funga za Sunnah na faida ipatikanayo kwa mwenye kufunga.
Kitabu cha V (IPC)
AKHLAQ Tabia Njema.
 • Ukweli.
 • Uaminifu.
 • Kuchunga ahadi.
 • Kauli njema.
 • Unyenyekevu.
 • Huruma (ukarimu).
 • Upendo.
 • Haya.
 • Subra.
 • Kusamehe.
 • Ujasiri.
 • Kutosheka (kukinai).
 • Utii na Heshima
Awe na tabia njema.
 • Mwalimu abainishe vipengele hivi vya tabia njema kwa aya za Qur-an na Hadithi.
 • Aonyeshe umuhimu wa kujipamba na tabia njema.
Kiabu cha V (IPC)
Vyakula Halali.
 • Kuchinja Kiislamu.
 • Wanyama walioharamishwa kuliwa.
 • Hekima ya kukataza kula kwa makafiri na washirikina.
 • Ahlul-kitaab.
Aweze kupambanua vyakula halali na haramu.
 • Mwalimu aonyeshe namna ya kuchinja kwa kuonyesha mfano.
 • Aorodheshe wanyama walioharamishwa.
 • Aonyeshe hekima ya Waislamu kutokula kwa wasiokuwa Waislamu.
Kitabu cha V (IPC)
TAREKH Historia ya Mwanaadamu.
 • Asili ya mwanaadamu.
 • Lengo la kuumbwa mwanaadamu.
 • Hadhi yake hapa ulimwenguni.
 • Kuwepo Elimu na mwongozo.
Aweze kueleza asili ya mwanaadamu, lengo la maisha yake na Hadhi yake hapa ulimwenguni.
 • Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa kurejea Qur-an na Hadithi asili ya mwanaadamu, lengo la kuumbwa kwake na Hadhi yake.
 • Abainishe kuwa Elimu na mwongozo wa Qur-an na Sunnah ndio nyenzo zinazomuwezesha mwanaadamu kuwa Khalifa na kufikia lengo la maisha yake.
Kitabu cha V (IPC)
Historia ya Mitume wa Allah (S. W.)
 • Adam (A. S)
 • Nuhu (A. S)
 • Idrisa (A. S)
 • Swalehe (A. S)
 • Ayubu (A. S)
 • Yunus (A. S)
 • Ibrahim (A. S)
 • Lut (A. S)
 • Ismaili na Is-haq (A. S)
 • Yaquub (A. S)
 • Yusufu (A. S)
 • Musa na Harun (A. S)
 • Daud (A. S)
 • Suleiman (A. S)
 • Isa (A. S)
Aweze kueleza ujumbe wa Mitume kwa wanaadamu, upinzani dhidi yao na wafuasi wao, subira yao na ushindi dhidi ya maadui zao, mafundisho yapatikanayo.
 • Mwalimu aeleze historia ya Mitume kwa kurejea Qur-ani.
 • Abainishe mafunzo yatokanayo na historia ya kila Mtume.
Kitabu cha V (IPC)

Muhtasari kwa madarasa mengine

Home Darasa la Kwanza Darasa la Pili Darasa la Tatu Darasa la Nne Darasa la Sita Darasa la Saba

Muhtasari huu umetayarishwa na Islamic Propagation Centre, S. L. P. 55105, Dar es salaam, Tanzania
1