Methali za kiswahili


1 Asifuye mvuwa imemnyea. Akili nyingi huondowa maarifa.
2.Asiye kubali kushindwa si mshindani.
3.Atangaye na jua hujuwa. Asiye kuwapo na lake halipo.
4.Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo. Baada ya dhiki faraja. Baniani mbaya kiatu chake dawa.
5.Bendera hufuata upepo. Bilisi wa mtu ni mtu..
6.Chamlevi huliwa na mgema.
7.Chanda chema huvikwa pete..
8.Chombo cha kuzama hakina usukani.Chovya - chovya yamaliza buyu la asali.
9.Dalili ya mvua mawingu.
10.Damu nzito kuliko maji.
11.Dawa ya moto ni moto.
12.Dua la kuku halimpati mwewe..
13.Fadhila ya punda ni mateke. Fimbo ya mbali hayiuwi nyoka..
14.Fuata nyuki ule asali.
15.Fumbo mfumbe mjinga mwerevu huligangua.
16.Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.
17.Haba na haba hujaza kibaba.
18.Hapana marefu yasio na mwisho.
19.Hakuna siri ya watu wawili.
20.Haraka haraka haina baraka
21.Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
22.Kelele za mlango haziniwasi usingizi.
23.Kenda karibu na kumi.
24.Kiburi si maungwana.
25.Kichango kuchangizana.
26.Kidole kimoja hakivunji chawa.
27.Kingiacho mjini si haramu.
28.Kikulacho ki nguoni mwako.
29.Kila chombo kwa wimblile.
30.Kila mlango na ufunguwo wake.
31.Kila mtoto na koja lake.
32.Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake..
33.Kila ndege huruka na mbawa zake.
34.Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.
35.Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
36.Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
37.Kinyozi hajinyoi.
38.Kinywa ni jumba la maneno.
39.Kipendacho moyo ni dawa.
40.Kipya kinyemi ingawa kidonda.
41.Kisebusebu na roho kipapo.
42.Kisokula mlimwengu,sera nale.
43.Kitanda usicho kilala hujui kunguni wake.
44.Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
45.Kiwi cha yule ni chema cha;hata ulimwengu uwishe.
46.Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
47.Konzo ya maji haifumbatiki.
48.Kosa moja haliachi mke.
49.Kozi mwandada ,kulala na njaa kupenda.
50.Kuagiza kufyekeza.
51.Kuambizana kuko kusikilizana hapana.
52.Kucha M'ngu si kilemba cheupe.
53.Kuchamba kwingi,kuondoka na mavi.
54.Kufa kufaana.
55.Kufa kwa jamaa, harusi.
56.Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika.
57.Kuishi kwingi ni kuona mengi.
58.Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele.
59.Kukopa harusi kulipa matanga.
60.Kuku havunji yai lake.
61.Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
62.Kula kutamu ,kulima mavune.
63.Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
64.Kunako matanga kume kufa mtu.
65.Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
66.Kupanda mchongoma ,kushuka ngoma.
67.Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
68.Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
69.Kutu kuu ni la mgeni.
70.Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
71.Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
72.Kwenda mbio siyo kufika.
73.Kwenye miti hakuna wajenzi.
74.La kuvunda(kuvunja) halina rubani.
75.La kuvunda (kuvunja)halina ubani.
76.Lake mtu halimtapishi bali humchefusha.
77.Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
78.Liandikwalo ndiyo liwalo.
79.Lila na fila hazitangamani.
80.Lipitalo ,hupishwa .
81.Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
82.Lisilokuwapo moyoni,halipo machoni.
83.Maafuu hapatilizwi.
84.Macho hayana pazia.
85.Mafahali wawili hawakai zizi moja.
86.Maiti haulizwi sanda.
87.Maji hufuata mkondo.
88.Maji huteremka bondeni,hayapandi mlima.
89.Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaogelea.
90.Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
91.Maji ya kifufu ni bahari ya chungu.
92.Maji yakija hupwa.
93.Mpanda ngazi hushuka.
4.Maji yakimwagika hayazoleki.
95.Majumba makubwa husitiri mambo.
96.Majuto ni mjukuu.
97.Manahodha wengi chombo huenda mrama.
98.Maneno makali hayavunji mfupa.
99.Maneno mema hutowa nyoka pangoni.
100.Masikini akipata matako hulia mbwata.
101.Masikini haokoti,akiokota huambiwa kaiba.
102.Masikini na mwanawe tajiri na mali yake.
103.Mavi usioyala,wayawingiani kuku?
104.Mavi ya kale hayanuki.
105.Mbinu hufuata mwendo.
106.Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
107.Mbiu za mgambo ikilia kuna jambo.
108.Mchagua jembe si mkulima.
109.Mchagua nazi hupata koroma.
110.Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.
111.Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo.
112.Mchelea mwana kulia hulia yeye..
113.Mchele moja mapishi mengi.
114.Mcheka kilema hafi bila kumpata.
115.Mcheza hawi kiwete,ngoma yataka matao.
116.Mcheza kwao hutuzwa.
117.Mcheza na tope humrukia.
118.Mchezea zuri ,baya humfika.
119.Mchimba kisima hungia mwenyewe.
120.Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
121.Mchovya asali hachovi mara moja.
122.Mchuma janga hula na wakwao.
123.Mchumia juani,hula kivulini.
124.Mdharau biu,hubiuka yeye.
125.Meno ya mbwa hayaumani.
126.Mfa maji hukamata maji.
127.Mficha uchi hazai.
128.Mfinyazi hulia gaeni.
129.Mfuata nyuki hakosi asali.
130.Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
131.Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
132.Mganga hajigangui.
133.Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
134.Mgeni ni kuku mweupe.
135.Mgeni njoo mwenyeji apone.
136.Mgonjwa haulizwi uji.
137.Miye nyumba ya udongo ,sihimili vishindo
138.Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
139.Mjumbe hauawi.
140.Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
141.Mkamia maji hayanywi.
142.Mkata (masikini) hana kinyongo.
143.Mke ni nguo ,mgomba kupalilia.
144.Mkono moja hauchinji ngombe.
145.Mkono moja haulei mwana.
146.Mkono mtupu haulambwi.
147.Mkono usioweza kuukata,ubusu.
148.Mkosa kitoweo humangiria.
149.Mkuki kwa nguruwe mtamu,kwa mwanadamu uchungu.
150.Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
151.Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
152.Mla cha uchungu na tamu hakosi.
153.Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekeya.
154.Mla mbuzi hulipa ngombe.
155.Mla mla leo mla jana kala nini?
156.Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
157.Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
158.Mlimbua nchi ni mwananchi.
159.Mnyamaa kadumbu.
160.mnywa maji kwa mkono moja,Kiu yake i pale pale.
161.Moja shika,si kumi nenda urudi.
162.Moto hauzai moto.
163.Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
164.Mpanda ovyo hula ovyo.
165.Mpemba akipata gogo hanyii chini.
166.Mpemba hakimbii mvua ndogo.
167.Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
168.Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia.
169.Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
170.Msasi haogopi mwiba.
171.Msema pweke hakosi.
172.Mshale kwenda msituni haukupotea.
173.Mshoni hachagui nguo.
174.Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
175.Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
176.Mstahimilivu hula mbivu.
177.Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
178.Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
179.Mtaka unda haneni.
180.Mtaka yote hukosa yote.
181.Mtegemea nundu haachi kunona.
182.Mtembezi hula miguu yake.
183.mteuzi hashi tamaa.
184.Mti hauwendi ila kwa nyenzo.
185.Mtondoo haufi maji.
186.Mtoto akililia wembe mpe.
187.Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
188.Mtoto wa nyoka ni nyoka.
189.Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
190.Mtu hujikuna ajipatiapo.
191.Mtu huulizwa amevaani ,haulizwi amekulani.
192.Mtumai cha ndugu hufa masikini.
193.Mtumi wa kunga haambiwi maana.
194.Mtumikie kafiri upate mradi wako.
195.Mtupa jongoo hutupa na mti wake.If you throw a millipede you should throw away the stick you picked it up with
196.Mume wa mama ni baba.
197.Mungu hamfichi mnafiki.
198.Mvumbika changa hula mbovu.
199.Mvungu mkeka.
200.Mvunja nchi ni mwananchi.
201.Mvuvi ajuwa pweza alipo.
202.Mwacha asili ni mtumwa.
203.Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
204.Mwamini Mungu si mtovu.
205.Mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
206.Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
207.Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.
208.Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
209.Mwana simba ni simba.
210.Mwanga mpe mtoto kulea.
211.Mwangaza mbili moja humponyoka.
212.Mwanzo kokochi mwisho nazi.
213.Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
214.Mwanzo wa ngoma ni lele.
215.Mwapiza la nje hupata la ndani.
216.Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
217.Mwenda bure si mkaa bure,huenda akaokota.
218.Mwenda mbio hujikwa kidole.
219.Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.
220.Mwenye kelele hana neno.
221.Mwenye kovu usidhani kapowa.
222.Mwenye kubebwa hujikaza.
223.Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
224.Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka.
225.Mwenye macho haambiwi tazama.
226.Mwenye nguvu mpishe.
227.Mwenye njaa hana miiko.
228.Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
229.Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
230.Mwenye shoka hakosi kuni.
231.Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja. i hushikwa na mwizi mwenziwe.
232.Mwomba chumvi huombea chunguche.
233.Mwosha hadhuru maiti.
234.Mwosha huoshwa.
235.Mwosha husitiri maiti.
236.Mzaha,mzaha, hutumbuka usaha.
237.Mzazi haachi ujusi.
238.Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia usufi.
239.Mzika pembe ndiye mzua pembe.
240.Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
241.Mzowea kunyonga, kuchinja hawezi.
242.Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
243.Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
244.Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona.
245.Nazi mbovu harabu ya nzima.
246.Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu,
247.Ndege mwigo hana mazowea.
248.Ndugu chungu, jirani mkungu. (Alt. Ndugu kitu.... .)
249.Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
250.Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
251.Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
252.Ngoma ivumayo haidumu.
253.Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
254.Ngozi ivute ili maji.
255.Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu.
256.Nifae na mvua nikufae na jua.
257.Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
258.Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili.
259.Njia ya mwongo fupi.
260.Njia ya siku zote haina alama. A regular path has no signpost. cf. A used key is always bright.
261.Ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
262.Ng'ombe haelemewi na nunduye.
263.Nta Si asali; nalikuwa nazo Si uchunga. 264.Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
265.Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.
266.Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
267.Nyumba ya udongo haihimili vishindo.
268.Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu. Pabaya pako Si pema pa mwenzako.
269.Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako.
270.Painamapo ndipo painukapo.
271.Paka akiondoka, panya hutawala. Paka hakubali kulala chali.
272.Paka wa nyumba haingwa.
273.Panapo wengi hapaharibiki neno.
274.Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
275.Pele hupewa msi kucha.
276.Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
277.Penye kuku wengi hapamwagwi mtama.
278.Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
279.Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/na mwema wako hakosi.
280.Penye miti hakuna wajenzi.
281.Penye nia ipo njia.
282.Penye urembo ndipo penye urimbo.
283.Penye wazee haliharibiki neno.
284.Penye wengi pana mengi.
285.Penye wengi pana Mungu.
286.Pilipili usozila zakuwashiani?
287.Pofu hasahau mkongoja wake.
288.Pwagu hupata pwaguzi.
289.Radhi ni bora kuliko mali
290.Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
291.Samaki mmoja akioza, huoza wote. I
292.Shika! Shika! na mwenyewe nyuma.
293.Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
294.Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
295.Si kila mwenye makucha huwa simba.
296.Sikio halilali na njaa.
297.Sikio halipwani kichwa. Alt: Sikio halipiti kichwa.
298.Sikio Ia kufa halisikii dawa.
299.Siku njema huonekana asubuhi.
300.Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
301.Simba mwenda kimya(pole) ndiye mla nyama.
302.Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.
303.Sitafuga ndwele na waganga tele.
304.Subira ni ufunguo Wa faraja.
305.Subira yavuta heri, huleta kilicho mbali.
306.Sumu ya neno ni neno.
307.Tamaa mbele, mauti nyuma.
308.Taratibu ndiyo mwendo.
309.Teke Ia kuku halimwumizi mwanawe
310.Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.
311.Uchungu wa mwana, aujua mzazi.
312.Udongo uwahi ungali maji
313.Udugu wa nazi hukutania chunguni
314.Ukenda kwa wenye chongo, vunja lako jicho.
315.Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea. Ukiona neno, usiposema neno, utapatikana na neno.
317.Ukiona zinduna, ambari iko nyuma.
318.Ukipewa shibiri usichukue pima.
319.Ukupigao ndio ukufunzao.
320.Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.
321.Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
322.. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliyeno,na.
324.Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa.
325.Ulimi hauna mfupa.
326.Ulimi unauma kuliko meno.
327.Ulipendalo hupati, hupata ujaliwalo.
328.Ulivyoligema utalinywa.
329.Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?
330.Umekuwa bata akili kwa watoto?
331.Umekuwa jeta hubanduki?
332.Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
333.Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
334.Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
335.Ushikwapo shikamana.
336.Usiache kunanua kwa kutega.
337.Usiache mbachao kwa msala upitao.
338.Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
339.Usigombe na mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
340.Usijifanye kuku mweupe.
341.Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno watafune.
342.Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
343.Usimwamshe aliyelala utalala wewe.
344.Usinivishe kilemba cha ukoka.
345.Usipoziba ufa utajenga ukuta.
346.Usisafiriye na nyota ya mwenzio.
347.Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
348.Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu.

BACK TO MAIN PAGE

أفلاج بني قتب Aflag Bani Qatab