MAFUNDISHO
BWANA YESU ANAKUJA: MAMBO YA MUHIMU SANA KUJISHUGHULISHA NAYO KWA SIKU HIZI
You need Java to see this applet.
Kuwasiliana nami, andika kwa.......
RUDI " NAIOTH" - HOMEPAGE
...Inatoka uk.2
                                                        MUNGU ANAJALI MAOMBI

Unajua, Machozi yanaleta tofauti kabisa katika hali ya aina fulani!  Machozi yamezungumzwa mno katika maandiko, bali ni mara chache sana tunayaona mle – tunapita juu juu!
Ni mara tu wana wa Israeli walipougua na kulia kwa maumivu – ndipo Mungu alipokuja na kuwasikia.  Alisema
“
Nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nimekuona kuugua kwao, hivyo nimekuja kuwaokoa" (linganisha na Mdo 7:34).
Neno “
kuugua” linapotumika hapa ni muhimu sana.  Linalingana na lile lililotumika kwa Roho Mtakatifu kuwa anapotusaidia udhaifu wetu anaugua (War. 8:28).

Neno kusaidia lilipotumika katika Warumi 8:28 limetumika mara nyingine chache sana katika Agano Jipya.  Sehemu nyingine ni pale Martha alipokuja kwa Yesu na kulalamika kuhusu Mariamu – kuwa aende amsaidie!  Alisema kama hivi:
  “
Mshurutishe anisaidie” –au “Mshurutishe ajihusishe”.
Maana inayoletwa hapa ni kuwa umebeba mzigo mzito, na unapokaribia
KARIBU SANA na kuuangusha ninakuja kukusaidia kabla HUJAVUNJIKA!

Roho wa Mungu hutusaidia udhaifu wetu.  Anakuja kunisaidia kwa
KUUGUA.  Neno hili limetumika tena katika Matendo 7 – kwenye hotuba ya Stefano wakati alipoelezea kuugua kwa wana wa Israeli wakitamani mtu awaokoe toka utumwani – toka matesoni – toka vifungoni!  Ni aina hii hii ya kuugua aliyokuwa nayo  Hana mkewe Elikana, na Bwana  akampatia mtoto – Nabii Samweli (1Samweli 1:1-20)

Ndipo kuugua ambako Isaya alimwona Hezekia akitokwa machozi na Mungu akasema kuwa
AMEYAONA MACHOZI YAKE,  naye atabadili mauti aliyokusudia kuwa uzima (2Waf. 20:5).

Nehemia alikuwa akilia kwa machozi.  Macho yake yaliyovimba, na uso ulio na simanzi na machozi vikaonekana kwa mfalme. Mungu aliyatumia machozi yake kuwa ukombozi wa watu wake na Ujenzi wa ukuta wa Yerusalemu. 
Mara kwa mara tunasoma kuwa Mungu hataidharau roho iliyonyenyekea na kupondeka.
Zab. 6:8 tunasoma kuwa Bwana alisikia sauti ya kuugua kwa mtu wa Mungu.

                                                              
PANDA KWA MACHOZI

Neno lasema kuwa lazima tupande kwa machozi. Panda Neno la Mungu kwa machozi. Mkumbuke Mtume Paulo.  Anasema katika Mdo 20 kuwa alikuwa na Waefeso miaka mitatu usiku na Mchana, na aliwahubiria Neno kwa machozi. 
PAULO ALIHUBIRI KWA MACHOZI.
Katika 2Wakor. 2:4 anasema kuwa
ALIANDIKA WARAKA KWA MACHOZI kwenda Korintho.  Anapomwandikia Timotheo anamwambia kuwa AMAYAKUMBUKA MACHOZI YAKE (2Tim.1:4)

Tukajifunza kupanda kwa machozi katika vyumba vyetu vya maombi, tukatoka na mioyo iliyopondeka tutaona matunda ya ahadi za Mungu kwa yale tuliyoyanena kwa Imani!
Haya ndiyo maandalizi ya kweli ya Mtumishi wa Mungu –
KUMPA MUNGU AKILI NA MOYO WAKO AUTUMIE.

                                                                 
MTUMIKIE MUNGU KWA MACHOZI
Paulo pia alitumika kwa Machozi.
Mdo 20:19 Paulo anaelezewa kuwa
ALITUMIKA KWA MACHOZI MENGI.  Maana ya utumishi kwa machozi mengi labda tunaifahamu kidogo sana!

Nadhani maana ya
KUTUMIKA KWA MACHOZI ni kumtumikia Mungu kukubali kupata mateso pamoja naye!  Unaonaje?    Ukapata msiba mkubwa na  mtu mmoja akakujia, akaketi na wewe na kuugua na wewe, je  amefanya huduma yoyote kwako?
Naona hivyo hivyo. Tunaamka kwenda kumtumikia Mnahudumu mbele yake, unaugua kwa yale anayougua, tunabeba mzigo ule anaoubeba, tunawapenda wale anaowapenda – tunamtumikia Mungu kwa namna ya kuwa
WATENDAKAZI PAMOJA NAYE – huu ni UTUMISHI WA MACHOZI (linganisha 1Wakor. 3:9).  Haiwezekani ukatumika hivyo na macho makavu!

Hutalia tu kwa hali ile Mungu anayoililia pia, utaulilia udhaifu wa Kushindwa kwako pia!
Unajua, tunatamani sana
nguvu za Mungu bali hatutaki Maumivu yake!

Wafilipi 3:10 tunajifunza kitu kinachoitwa
USHIRIKA WA MATESO ambao Paulo aliutamani “MATESO” hapa ni wingi – sio umoja! Paulo alijieleza kuwa alikuwa MWENYE HUZUNI lakini siku zote mwenye furaha.  2Wakor. 6:10.
Huu ndio wito wetu.  Hivi tumevitupa wapi hivi – Ule uzuri wa kukaa kimya mbele za Mungu, kuuingia moyo wake na kujimwaga mbele za uwepo wake; na kumtumikia kwa Machozi?  Kwenye
HUDUMA YAKE tusisahau HUDUMA KWAKE!
Jua Moyo wa Mungu.
...Inaendelea