Hali ya barabara za Dar es Salaam kwa wapanda baisikeli
Barabara ya Morogoro
- Hakuna njia hasa kwa wapanda baisikeli - wako pamoja na watembea kwa miguu
- Karibu na Ubungo na stand ya mkoa kuna wafanyabiashara wengi wanaziba njia
- Eneo la Tip Top na Manzese kuna wafanyabiashara na stand zao wanaziba njia
- Eneo la Jangwani kuna karavat na madaraja madogo yameharibika - lazima kushuka kwenye baisikeli na kupanda tena mara nyingi. HABARI - mwezi wa sita mwaka 2006 matatizo haya yamerekebishwa.
- Eneo la Fire kuna teksi nyingi wamepaki njiani
- Eneo la mjini mtaa ni mwembamba sana
Barabara ya Kawawa
- Hakuna njia hasa kwa wapanda baisikeli - wako pamoja na watembea kwa miguu
- Kati ya Kigogo na Msimbazi kwenya upanda moja njia ni embamba sana mpaka baisikeli haiwezi kupita
- Maeneo ya vituo vya mabasi njia inapita mbele ya vituo siyo nyuma na ni ngumu kwa baisikeli kupita katika watu wengi wanaosubiri. Karibu kila kituo ni nguma kupita.
- Teksi na lori wanapaki njiani
- Kinondoni kuna wafanyabiashara wengi njiani wanaziba njia
- Magomeni kuna nguzo kuziba magari kuingia njiani - hii ni nzuri
- Kati ya Mtaa Uhuru na Barabara Nyerere kuna vitu vinasababisha pancha
Barabara ya Nyerere
- Kati ya ilala na kariakoo kuna njia nzuri upanda moja - imelindwa kutoka magari, kuna sehemu ya baisikeli na watembea kwa miguu, kuna miti kwa kivuli
- Njia ya baisikeli inapita nyuma ya kituo cha dala dala cha darajani - nzuri
- Hakuna alama kuonyesha wapi ni njia ya baisikeli, kuna lami tofauti tu, watembea kwa miguu hawawezi kujua
- Kuna nguzo zinaziba magari kuingia njiani - nzuri
- Karibu ya kariakoo lami ya njia ni mbovu
- Baada ya Mtaa Mzimbasi kuna misingi kubwa - lazima baisikeli inatumia njia ya magari si ya baisikeli
Barabara ya Nelson Mandela
- Sehemu ningine kuna njia ya baisikeli na watu, sehemu ningine hakuna kabisa (kama kati ya gereji na Mabibo External)
- Sehemu ningine njia ni ya vumbi, ina mashimo mengi, kuna tupu na mchango ningi. Tabata kuna shimo kubwa inasababisha kushuka baisikeli
- Seheum ningi lori zinapaki njiani kama Vingunguti, Gereji, Mabibo External
- Tabata njia ni embamba sana mpaka baisikeli haiwezi kupita mtembea kwa miguu
- Riverside ni ngumu kupita kituo cha dala dala
- Karibu na Ubungo kuna wafanyabiashara wengi njiani
Barabara ya Ali Hassan Mwinyi
- Njia kupita Upanga ni nzuri, hakuna misingi kubwa, kuna nguzo kuziba magari kuingia njiani, kuna miti inyotoa kivuli
- Baisikeli na watembea kwa miguu wanatumia njia moja
- Kituo cha mabasi cha Aga Khan na Palm Beach kuna watu wengi, ngumu kupita
- Palm Beach teksi zinapaki njiani
- Kuingia njia ya baisikeli na miguu ya daraja ya selenda lazima kushuka baisikeli kwa sababu ya misingi kubwa
- Lami ya njia imeharibika sana kati ya daraja ya selenda na Ubalozi wa Ufaransa
- Lazima kushuka baisikeli kuvuka Barabara ya Kinondoni kwa sababu ya misingi kubwa
- Kuna kitu kinasababisha pancha baada ya Ubalozi wa Ufaransa
- Njia nzuri kati ya Ubalozi na Best Bite hata kama watembea kwa miguu na wapanda baisikeli wanatumia njia moja
- Kati ya Best Bite na Morocco magari mengi yanapaki njiani yanaziba njia kabisa
Old Bagamoyo Road
- Hakuna njia ya baisikeli wala ya watembea kwa miguu
Barabara ya Chang'ombe
- Hakuna njia ya baisikeli wala ya watembea kwa miguu