CHUO KIKUU
‘FRESH’
WATAKIWA KUACHA
KUPENDA NGONO
NIPASHE,
Jumatano Septemba 21,2005
Na Richard Makore
                                 

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wameshauriwa kuacha tabia za kppenda ngono kuliko masomo ili waweze kujiepusha na maambukizi ya Ukimwi.

Ushauri huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na mmoja wa vijana kutoka mtando wa ushirikiano wa wanafunzi dunian SPW,
Bw Shikunzi John katika hafla ya kuwakaribisha wanafunziwa mwaka wa kawanza Chuo Kikuu ehemu ya Mlimani.

Bw.John alisema, sual la ukimwi lipo na ni kubwa has katika vyuo vinavyotoa elimu ya juu hivyo ili kujiinga na janga hilo lazima vijana has wa kie kuacha tabia za tamaa za vitu.

Alisema asilimia kubwa ya wanafunzi wanaojinga na Chuo wana umri mdogo ambao ndiyo wanaokabiliwa na gonjwa hilo la hatari hivo lazima wajue na kuchukua tahadhari za hali ya juu.

Alisema SPW ni mtandao ambao unafanya kazi ya kujitolea kwa ajili ya utoaji wa elimu juu ya Ukimwi na malezi bora ya vijana hivyo kwa wanafunzi hao wapya ni boara wakaulumia katika kupata taarifa muhimu juu ya ugojwa huo.

Aliongeza kuwa endapo wanafunzi watakubali kupatiwa elimu juu ya ukimwi ana imani watamalilza masomo yalo kwa imani watamaliza masomo yao kwa amani na kutunukiwa Shahada lakini ikiwa itakuwa kinyume chake watatunukiwa “Shahada ya HIV,” alisema Bw John.

Naye mwanafunzi anayesoma chuoni hapo mwaka wa nne
Bi Theresia Moyo, aliwataka wanafunzi kulinda na kuenzi maadili waliyotokanayo shuleni ili iwe kinga yao dhidi ya kuambukizwa ukimwi.

Alisema kuwa maisha ya Chuo yana uhuru zaidi kuliko ya shule hali ambayo wasipokuwa makini inaweza kuwasababishia madhara makubwa katika maisha yao.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mratibu Msaidizi wa SPW,
Bi Grace Simba alisema shirika lake linafanya kazi ya kutoa elimu ya Ukimwi na malezi bora kwa vijana wa rika zote kuanzia shule vyoo na hata mitaani.

Alisema elimu hiyo hutolwa kwa njia ya tovuti na vipeperushi mbaimbali vilivyona ujumbe juu ya ugonjwa wa ukimwi ndani na nje ya nchi kwa lengo la kutunza maisha ya vijana.

 

 Je, unajua kuhusu Huruma Africares Foundation? Ni Asasi isiyokuwa ya Kiserikali, Pamoja na mambo mengine tunayofanya. Tunashughulika na yafuatayo ambayo tunayaandika baadhi yake tu kwa lugha ya Wazungu. Aidha wasiliana nasi tufanye kazi wote

What does Huruma Africares Foundation does ?

To provide a forum for information exchange among Tanzanian nationals and other interested person through various mode of communication including the worldwide Internet. Discussion in the forum shall be open and not restricted to any particular subject or topic, but strong emphasis shall be placed on issues related to the enhancement of the quality of life of Tanzanians

 

Home
 
Cut a tree plant Trees
 

Tumeharibu mazingira