English version

Umma wa Wapanda Baiskeli Dar es Salaam

Dar es Salaam

Utambulisho

Jiunga na UWABA!

Mkutano wa UWABA

Rudi juu

Mikutano

Tunakutana ofisini kwetu (Manzese, Sisi kwa Sisi) kila jumamosi saa nne asubuhi
Hakuna kiingilio cha kulipa, ni bure kujiunga.
Wapanda baiskeli wote mnakaribisha. Ukisikia mtaarifu mwenzio.
Wanachama 152 wamejiunga mpaka sasa.

Mkutano wa UWABA

Rudi juu

Habari

UWABA tunakutana na JICA

Tarehe 1 Juni 2009, wanachama wa UWABA walikutana na wafanyakazi wa Japanese International Cooperation Agency (JICA). Tuliongeana kuhusu Barabara ya Kilwa, ambayo JICA walidhamini, na Dar es Salaam Transport Master Plan, na vipi mazingira na usalama wa wapanda baisikeli na usafiri wa siyo ya moto unaweza kuboreshwa.

UWABA tunahudhuria mikutano

Tarehe 28 Mei 2009, wanachama wawili wa UWABA walihudhuria mkutano huko Tanga kuhusu "Urban Development and Environmental Management" (maendeleo ya jiji na mazingira), ambapo pia diwani wa halmashauri ya Tanga walihudhuria. Kwenye mkutano huu, UWABA tulichangia mawazo kuhusu vipi uhamasishaji wa baisikeli kama chombo cha usafiri unaweza kufanya jiji lipendeze na liwe jiji la watu siyo jiji la magari. UWABA pia tulimpa Meya wa Tanga, Mhe. Kisauji, helmeti na jaketi ya reflecta.

UWABA tunampa helmeti na reflecta jaketi kwa Mhe Kisauji, Meya wa Tanga

Tarehe 7-8 Mei 2009, mwenyekiti wa UWABA alihudhuria mkutano wa NGOs wanaofanyakazi katika kuboresha usalama barabarani, huko Brussels, Ubeljiji. Mkutano ulitayarishwa na shirika la afya duniani (World Health Organisation). Alitoa mada kuhusu kazi ya UWABA kuleta usalama barabarani kwa wapanda baisikeli wa Dar es Salaam. Mkutano huu umetengeneza mapendekezo kwenda kwa mkutano wa mawaziri wa usalama barabarani Moscow mwisho wa mwaka huu. UWABA tulisaidia kuhakikisha kwamba mapendekezo kulinda wapanda baisikeli na watembea kwa miguu, na miundombinu inayowalinda, yawe humu. Mada ya UWABA ipo kwenye tovuti ya WHO .

Tarehe 21-23 Oktoba 2008, mwenyekiti wa UWABA chairman alihudhuria mkutano wa mradi wa umoja wa taifa wa mazingira (United Nations Environmental Program) kuhusu ubora wa hewa jijini huko Nairobi, Kenya. Kwenye mkutano huu alieleza vipi kuhamasisha baisikeli kama chombo cha usafiri unaweza kusaidia kuboresha ubora wa hewa jijini.

UWABA tunafundisha usalama wa baiskeli shule za Msongola na Kigamboni, na kwa wapanda baisikeli Magomeni

Mafunzo ya usalama wa baisikeli shule ya Kigamboni

UWABA tunaendelea vizuri na mradi wetu wa usalama wa baiskeli, chini ya Wamba Memorial Fund.

Tarehe 6 na 13 Juni 2009, wanachama wa UWABA ambao wameshahudhuria mafunzo ya wakufunzi, walifundisha wapanda baisikeli wenzao 24 kwa kutumia darasa na uwanja wa shule ya Nyerere, Magomeni. Diwani wa Kata ya Makurumla (Ndugu Rajabu) na Diwani wa Manzese (Ndugu Manumbu) walikuwa wageni rasmi.

Tarehe 21 na 28 Februari 2009, wanachama wanne wa UWABA walifundisha usalama wa baisikeli kwa wanafunzi 37 wa Kigamboni Secondary School, Dar es Salaam. Mama Wamba alikuwa mgeni rasmi.

Tarehe 18 mpaka tarehe 21 Novemba 2008, wanachama sita wa UWABA walifundisha wanafunzi 60 wa sekondari na wanafunzi 55 wa shule ya msingi kwenye shule ya Msongola, Dar es Salaam. Wanafunzi, ambao wanakujaga shuleni na baiskeli, walishirikiana katika mafunzo ya darasa, vitendo na mazungumzo.


Cycle safety training in Msongola classroom

Video kuhusu baiskeli na usalama

Mwanachama wa UWABA Amar Shanghavi pamoja na wanachama wengine tumetengeneza video kuhusu UWABA na usalama wa baiskeli.

Msafara wa Baiskeli 2008

Diwani Lupilya Picha ndani ya gazeti ya Sunday Citizen

Msafara wa Baiskeli 2008 ulienda vizuri tarehe 25 oktoba 2008. Wapanda baiskeli 150 walishiriki. Mgeni rasmi Mhe Azzan Zungu mbunge wa Ilala alitoa hotuba kuhusu umuhimu wa baiskeli katika usafiri wa jiji na Diwani Lupilya wa Manispaa wa Ilala aliendesha baiskeli kwenye msafara na aliongea kwenye TV - Channel 10 na DTV. Mbalozi wa Ireland na mume wake waliendesha baiskeli pia. Tulikuwepo ukurasa wa kwanza kwenye Sunday Citizen. Zawadi za baiskeli tatu, baiskeli ya tairi tatu ya abiria, baisikeli ya mlemavu, helmeti 20 na jaketi za reflecta 20 zilitolewa kwa bahati nasibu na walioshinda walifurahi sana. Tunashukuru sana wadhamini wetu Ubalozi wa Ireland na waliochangia huduma/vifaa bure - Kampuni ya guta, Business Times, Manispaa ya Ilala na Ultimate Security. Tunatumaini tumewahi kuonyesha umuhimu wa baiskeli na usalama barabarani kwa wapanda baiskeli Dar es Salaam.Mkutano wa utawala wa sekta ya usafiri, Yaonde, Cameroon

Mejah akitoa maada kwenye mkutano

Tarehe 23-25 Septemba 2008 mwenyekiti wa UWABA, Mejah Mbuya, aliwakilishi UWABA kwenye mkutano wa utalawa wa sekta ya usafiri ya Afrika uliyotokea jiji la Yaonde, Cameroon. Mkutano uliendeshwa na shirika la gTKP. Mejah alitoa maada kuhusu ushirikiano wa UWABA na serekali.

Utafiti kuhusu usafiri wa baiskeli Dar es Salaam

Mwezi wa Septemba 2008 wanachama wa UWABA tumewasaidia watafiti Eyasu Markus Woldesmyas kutoka Ethiopia na Alphonse Nkurunziza kutoka Rwanda ambao wanafanya utafiti kwenye chuo cha ITC, Uholonzi. Utafiti wao ni kuhusu usafiri wa baiskeli Dar es Salaam na UWABA tumesaidia kufanya savei.

Tumehamia

Tarehe 1 Agosti 2008 UWABA tumehamia Manzese Sisi kwa Sisi, baada ya mkataba yetu ya kodi ya ofisi ya zamani ya Mabibo kumaliza. Karibu kutembelea ofisi, ambapo kuna taarifa nyingi kuhusu masuala ya baiskeli ya Dar es Salaam.

Mafunzo ya wakufunzi ya usalama wa baisikeli

Tarehe 21-23 julai 2008 UWABA tuliendesha kozi ya mafunzo ya wakufunzi ya usalama wa baisikeli Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mabibo. Mwalimu wetu alikuwa bwana Andrew Wheeldon kutoka Bicycling Empowerment Network, Afrika Kusini. Tulipata udhamini kutoka Wamba Memorial Fund kuendesha kozi hii pamoja na mradi wa usalama barabarani kwa wapanda baisikeli tunaoanza sasa. Mafunzo yalikuwa na washiriki 24 - mwakilishi kutoka TANROADS, mwakilishi kutoka Traffic Police, walimu watatu kutoka shule za Msongole na Kigamboni, wawakilishi wawili wa HUWATA na wanachama 14 wa UWABA. Washiriki hawa sasa wanatayarisha kutoa mafunzo haya kwa wanafunzi wa shule mbali mbali mkoa wa Dar es Salaam.

Picha ya wanachama wa UWABA anayetoa alama ya mkono ya kusimama

Uzinduzi wa Ofisi ya UWABA

Tarehe 19 aprili 2008 UWABA tulisherehe uzinduzi wa ofisi wetu. Wawakilishi wa SUMATRA na serekali za mitaa walikuwa wageni rasmi. Aidha tulitoa zawadi za helmeti, t-shirt na jaketi za njano kwa wanachama 27 wanaoshirikiana sana katika chama. Tunashukuru sana IBike / International Bicycle Fund merekani na La Stazione delle Biciclette wa Milan, Italia kwa ajili ya michango kubwa katika utengenezaji wa ofisi na zawadi.

UWABA office opening ceremony

Mkutano na mwakilishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

Tarehe 10 Machi 2008 wawakilishi watano wa UWABA tulikutana na Mama Mlamba, idara ya usafiri Halmashauri ya Jiji ya Dar es Salaam. Hapa unaweza kusoma habari ya mkutano huu:

Semina ya Usalama Barabarani - Chuo cha Taifa cha Usafirishaji

Tarehe 19 januari 2008 Chuo cha Taifa cha Usafirishaji waliendesha semina ya Usalama Barabarani kwa Wapanda baiskeli kwa wanachama 21 wa UWABA.

Washiriki na walimu wa Semina

Washiriki tulifundishwa kuhusu sheria na kanuni za usalama barabarani kwa wapanda baiskeli, alama na michoro ya barabarani na uendeshaji baiskeli kwa kujihami. Mafunzo ya muhimu tuliyopata yalikuwa kuhakikisha baiskeli ipo kwenye hali nzuri, vipi kuendesha baiskeli kwa usalama barabarani, umuhimu wa uheshima kati ya wanaotumia barabara, haki na wajibu wao kama ajali ikitokea, sheria za barabara, makutano ya barabara, mawasiliano barabarani na maana ya alama za barabara.

Mwisho wanachama wa UWABA walishukuru sana Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kwa kutoa hudumu hii nzuri kwa jamii ili kuongeza usalama barabarani kwa wapanda baiskeli. Mkuu wa Idara ya Usalama Barabarani, Bwana Chard Wemba alisema kwamba semina hii ni hatua ya kwanza na Chuo kitapenda kuendelea kushirikiana na UWABA kutoa mafunzo haya kwa wapanda baiskeli wengine.

Mkutano na Idara ya Usalama Barabarani ya Wizara ya Miundombinu

Tarehe 14 januari 2008 wawakilishi wanne wa UWABA tulikutana na Idara ya Usalama Barabarani ya Wizara ya Miundombinu. Kwa bahati mbaya mkutano huu haukuwa na mafanyiko kwa sababu tulipewa dakika 15 tu hata kama tulikuwa na miadi ya saa moja.

Mawasiliano na TANROADS

Mwezi wa kwanza 2008 tumepokea barua ya pili kutoka TANROADS ambayo inajibu maswali yetu ya ziada kuhusu barabara zinazojengwa upya - Barabara ya Sam Nujoma, Barabara ya Nelson Mandela na Barabara ya Kilwa. Jibu hili ilitusaidia na ilijibu maswali mengi. Pia, tulikutana na TANROADS makau makuu tarehe 27 Septemba kutoa mada. Tunaendelea kufuatilia utekelezaji wa mipango.

Hapa unaweza kuangalia jibu:

UWABA tunashirikiana katika Siku ya Uamsho wa Mabadiliko ya Majira

Nje ya ofisi ya Makamu wa Rais Mabadaliko ya majira ni suala muhimu kwa watanazania kwa sababu watanzania wengi wanategemea mvua kwa riziki yao. Wapanda baiskeli wanasaidia katika hiyo shida kwa kutotoa moshi ya carbon dioxide wakati wa kusafiri. Tarehe 8 Desemba 2007 UWABA tulishirikiana na Centre for Energy Environment Science & Technology (CEEST), Envirocare, Joint Environment and Development Management Action (JEMA), Journalists Environmental Association of Tanzania (JET), Legal and Human Rights Centre (LHRC), Tanzania Association of NGOs (TANGO), Tanzania Coalition for Sustainable Development (TCSD), Tanzania Traditional Energy Development and Environmental Organization (TaTEDO) na Tanzania Youth Environment Network (TAYEN) kuandaa msafara wa baiskeli kwa uamsho wa mabadaliko ya majira. Tulisafiri na baiskeli kutoka ofisini kwetu Mabibo mpaka ofisi ya Makamu Rais, ambapo tulitoa hotuba na tulikaribishwa na Kaimu Mkurugenzai Idara ya Mazingira Bwana Stephen Nkondokaya. Hatua kufuata tuliyopanga ilikuwa kusafiri na baiskeli mpaka Ubalozi wa Marekani kuwapa barua kutoka mashirika kumi. Lakini tulisimamishwa na polisi na tuliambiwa hatuwezi kuendelea kama kundi maeneo ya Ubalozi wa Marekani bila barua ya kutualika kutoka Ubalozi wa Marekani. Kabla ya msafara tulikuwa tumeshawapa taarifa kwa polisi na tulikuwa tumeshaomba Ubalozi wa Marekani kutupokea sisi na barua zetu siku ya uamsho wa mabadaliko ya majira, lakini inaonekana kwamba ubalozi hawapo tayari kusikia maoni yetu na hata walisimamisha msafara wetu. Tukio ilionyeshwa kwenye habari ya Channel 10 na katika gazeti la Majira, basi tunatumaini kwamba tulisaidia kutoa ujumbe kuhusu mabadaliko ya majira kwa viongozi wa mataifa wanaokutana jili la Bali, Indonesia.

Bonyeza hapa kupata taarifa zaidi:

Msafara wa Baiskeli Dar es Salaam 2007

UWABA pamoja na CHABADA tulikuwa na Msafara wa baiskeli mzuri tarehe 20 October 2007. Watu zaidi ya 200 walishirikiana katika msafara kutoka Mnazi Mmoja na kuzunguka Dar es Salaam. Wanawume, wanawake, vijana, walemavu na wazima walishirikiana. Mgeni rasmi wetu alikuwa Bwana Leonard Lupilya, diwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Kwenye hotuba tuliongea na tulisikia mambo ya usalama wa wapanda baiskeli, barabara salama kwa wapanda baiskeli na tulihamasisha baiskeli kama chombo kizuri cha usafari jijini. Zawadi za guta, baiskeli tatu, helmeti 20 na jaketi za njano 20 zilisambazwa kwa bahati nasibu kwa washiriki. Tunashukuru wadhamini wetu Ubalozi wa Uholonzi, Kampuni ya Guta, Kampuni ya Bakhresa, Ubalozi wa China, Clouds FM na Manispaa ya Ilala.

Msafara wa baiskeli

UWABA tuna ofisi

Tarehe 9 Augosti 2007 tumepata mchango ya Tsh 400,000 kutoka IBike / International Bicycle Fund na wanachama wetu wamechangia pia kupata ofisi ya UWABA. Ipo Mtaa wa Jitegemee, Mabibo. Kwa sasa tunatengeneza ofisi yetu iwe tayari kuweka taarifa nyingi kuhusu mambo ya baiskeli watu wasome. Pia tumenunua guta ya chama iweze kutupa mapato yakuendelea kukodi ofisi baadaye. Tunashukuru sana michango.

Tumefungua sanduka la posta

Tarehe 13 Augosti 2007 UWABA tumefungua sanduka la posta letu - ni SLP 90361, Dar es Salaam. Tunakaribisha mawasiliano kwa posta.

Mkutano na Carl Bro Associates, consultant ya Nelson Mandela Road

UWABA tulikutana na Carl Bro Associates, kampuni wanaofanya michoro ya Nelson Mandela Road, tarehe 12 julai 2007. Hapa unaweza kusoma dondoo:

Tumefungua akaunti ya benki

Tumefungua akaunti ya benki ya UWABA kwenye National Microfinance Bank tawi ya Magomeni. Namba ya akaunti yetu ni 2052300909.

Sehemu ya mikutano imebadilisha

Tumepata sehemu mpya ya mikutano - Mahakama ya Ndizi, Mabibo, kwa fundi guta karibu na Maktaba Baa. Sehemu hii inafaa sana kwa sababu kuna wapanda baiskeli na wapanda guta wengi katika eneo hili.

Mkutano na Manispaa ya Ilala kuhusu msongamano

Tarehe 15 Mei 2007 UWABA tulihudhuria mkutano wa manispaa wa Ilala kuhusu shida ya msongamano wa magari mjini. Tulitoa mawazo yetu kuhusu vipi baiskeli inaweza kusaidia katika tatizo hili na kuhusu shida kama magari mengi yanayopaki njiani.

Watu wapya kwenye kamati

Hongera Rashid Karanji na Sosthenes Amlima ambao wamechaguliwa kuwa kwenye kamati ya UWABA jumamosi 5 Mei 2007.

Swala la maguta

Wanachama wa UWABA pamoja na waendesha guta soko la Tandale tukisanya watu kusaini barua yetu

Tarehe 4 Aprili 2007 Manispaa ya Ilala walitangaza kwamba maguta hazitaruhusu tena kusafirisha bidhaa katika maeneo ya katikati ya jiji au Kariakoo. Sera hii ingeua biashara za watu wengi, ingeunda matatizo ya kusafirisha bidhaa na ingelete malori kubwa ningi mjini. Picha ya wanachama wa UWABA kwenye gazeti ya Dar Leo

UWABA tumepiga kampeni dhidi ya sera hii. Tumesanya watu 835 kusaini barua yetu inayoenda Manispaa ya Ilala. Tarehe 12 Aprili 2007 tulikutana na Meya wa Ilala kutoa maoni yetu. Tarehe 28 Aprili 2007 Meya ya Ilala ametangaza kwamba maguta na mikokoteni ni ruksa. Tunapongezi Meya kwa utawala bora wa kusikiliza maoni ya watu na kufanya uamuzi mzuri. Tutapenda kuendelea kusaidia Manispaa ya Ilala kurekebisha matatizo ya msongamano jijini.

Sehemu za kupaki baiskeli Mlimani City

Mlimani City Shopping Centre walikuwa wakikataa baiskeli kuingia sehemu yao ya kupaki magari, na askari wao kufika kazini kwa kutumia baiskeli. UWABA tuliwasiliana nao kulalamika kuhusu sera hii na wamekubali kubadilisha sera na kuweka sehemu ya kupaki baiskeli. Tutaendelea kufuatilia.

Mawasiliano na Waziri wa Miundombinu

Tumepata barua kutoka Waziri wa Miundombinu kusema anaunga mkono azma yetu kuunda asasi hii muhimu ya wapanda baiskeli.

Msafara wa baiskeli

UWABA tulishirikiana na AALOCOM na CHABADA kuandaa msafara wa baiskeli tarehe 14 oktoba 2006. Watu wengi walihudhuria na wote wamefurahi. Tulianza Mnazi Mmoja, tukazunguka na tulirudi tena Mnazi Mmoja. Polisi walifunga sehemu ya barabara kwa ajili yetu. Zawadi za baiskeli 5 mpya za California zilitolezwa kwa bahati nasibu. Mstahiki Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dr Mwilima alikuwa mgeni rasmi. Tunatumaini msafara wetu ulihamasisha matumizi ya baiskeli, ulihimiza uendeshaji wa baiskeli, ulizingatia usalama na ulihimiza serikali umuhimu wa kukuweka njia maalum za baiskeli.

Msafara wa baiskeli

Mkutano na TANROADS

Wanachama wa UWABA tulikutana na TANROADS mkoa wa Dar es Salaam tarehe 24 mei 2006. Tulitoa maada ya maoni yetu na tulionyesha picha za barabara tulizopiga. Hapa unaweza kuangalia maada yetu:

Tanzania Social Forum

UWABA tulihudhuria Tanzania Social Forum tarehe 22 mpaka 25 machi 2006 Mnazi Moja. Tumekutana na mashirika mengine na tumewapa watu wengi taarifa kuhusu sisi. Hapa kuna picha ya standi yetu:

UWABA kwenye Tanzania Social Forum

Tumesajiliwa

UWABA tumesajiliwa na Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto chini ya Non-Governmental Organisations Act, 2002. Namba yetu ni 02NGO/0683. Tulisajiliwa tarehe 23 februari 2006 na tulipewa cheti tarehe 2 machi. Pia tumejitambulisha kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam.

Rudi juu

Katiba

Rudi juu

Kamati

Rudi juu

Dondoo za mikutano

Mikutano yote inaendeshwa kwa kiswahili. Dondoo zinapatikana hapa.

Rudi juu

Taarifa kwa waandishi wa habari, kipeperushi, bango

Gazeti la Sunday Citizen wameshaandika makala kuhusu UWABA tarehe 12 machi 2006. Unaweza kusoma makala hii hapa:

Rudi juu

Matumizi ya baiskeli Dar es Salaam

UWABA tumeshirikiana na Robert Bartlett wa Schorrell Analysis ya Jerumani kutengeneza "The global book of transport - Chapter 2 - Tanzania, bicycles in Dar es Salaam". Unaweza kudownload document hii hapa:

Rudi juu

Mawazo yetu

Tuemandaa orodha zinazifuata:

Rudi juu

Picha

Tunasanya picha mbali mbali kama zinazifuata:

Rudi juu

Sheria na sera za Serikali za barabara na usafiri

Hapa unaweza kusoma sheria za barabara za Tanzania (Kiingereza)

Tumepata sheria hizi kutoka tovuti ya Bunge la Tanzania www.bunge.go.tz

Hapa unaweza kusoma sera ya Tanzania ya Usafiri (Kiingereza)

Rudi juu

Takwimu

Hapa kuna takwimu za ajali zilizohusika wapanda baiskeli mkoa wa Dar es Salaam:
MwakaIdadi ya AjaliIdadi ya VifoMajeruhiIdadi ya baiskeli
200532117300324
200631430306314

Tumepata taarifa hii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani, Kanda ya Dar es Salaam.

Rudi juu

Barabara za Dar es Salaam

Hapa kuna ramani ya barabara za Dar es Salaam.

Ramani ya Dar es Salaam

Tumepata ramani hii kutoka tovuti ya TANROADS www.tanroads.org

Rudi juu

Wasiliana nasi

baiskeli ya rangi

Rudi juu