TOP

PAGE3

I Previous page I Full page List I Next page

CONTENTS

Samples of Native Treaties (Africa in the 19th.century)/Mifano ya mapatano.(Africa karne ya 19 ya kristo)

  1. Treaty of Vivi(Congo) English and Kiswahili versions
  2. Treaty of theBritish Royal Niger Company English and Kiswahili versions

Treaty of Vivi

1.English version:

The Treaty of Vivi, June 13th, 1880.

From: Henry Wellington Wack "The Story of the Congo Free State" New York & London : Putnam 1905. For Internet Source see WHKLMA


2.Kiswahili translation:

Mapatano ya Vivi(Kongo) Juni 13, 1880.

Bwana August Sparhawk, wakili wa safari kati ya mataifa kuenda Kongo juu, kwa kuwa naibu na karani ya hesabu ya Comite d'etudes ya Kongo chini, pamoja na Vivi Mavungu, Vivi Mku, Ngusu Panda, Benzane Kongo, na Kapita, wote wamekutana katika stesheni ya Vivi tarehe 13,Juni, 1880 kushauriana na kuamua mashauri maalum yapasayo mambo ya ushirika. Baada ya ukaguzi tele, wamefikiana kwa madaraka na mipango yameyotiliwa humu mwafakani wa sasa, na hayo yasema;

  • Sharti la kwanza. - Hawa wakuu wa wilaya ya Vivi wameotajwa juu wajua kwamba Comite d'Etudes kukuanzisha na kukuza imara hasa za kutunza uchumi na biashara humu nchini zao ingekuwa kitu cha kupendezwa sana, na kuhakikisha nchi na wenyeji wake faida itakayotokea kwa kufanya hivyo. Kusudiana nia hii, wanaachia na wanatarakia Comite d'Etudes, yote yaliyomo kwa jumla ndani ya wilaya zao katikati ya mipaka yafuatayo: kwa kuenda magharibi, kasikazani, na mashariki, kingo za kushoto , mto wa Lulu, na kwa kuenda kusini, majimbo ya Kolu na Kongo.

  • Sharti la pili. - Wakuu wa wilaya ya Vivi wabainishe sawasawa kwamba majimbo haya yako sehemu kamili ya nchi zao, na wanaweza kutoyatumia bila zuio.

  • Sharti la tatu. - Ukomo wa majimbo yale yameyo kwisha ainishwa katika kifungu cha mwisho wa sharti la kwanza umekubaliwa kwa ajili ya lipo la bidhaa na vitu vya namna vifuatayo kwa kila mmojawao: Koti la rasmi , kofia , mkufu wa tumbawe, kisu ; na zawadi ya kanga mbili kila mwezi kwa Vivi Mavungu; kanga moja kwa Vivi Mku; kanga moja kwa Ngusu Mpanda; kanga moja kwa Benzane Kongo; kanga moja kwa Kapita.

  • Sharti la nne. - Ukomo wa nchi ni wakuiachiana, pamoja na wakupitisha haki zote za milki kwa Comite d'Etudes .

  • Sharti la tano. - Comite d'Etudes inaahidi wazi kuwaachia wenyeji wawe na furaha huru ya ardhi zao na wakujilimia hizi hata kupatia riziki zao. Inaahidi pia kulinda na kuhifadhi wao na mali zao ikiwa magomvi au maingizo yaijia kwa kipande chochote na uwezo wa kuushambulia uhuru wa binafsi wao, au ikiwa kutwaa mazao ya kazi zao kwao.

  • Sharti la sita. - Wakuu wa wilaya ya Vivi wakubali tena kuwapa Comite d'Etudes- (1)Ukomo wa njia zote za mawasiliano ambazo ziko wazi sasa, au zitawazishwa katika eneo lote la nchi zao. Comite d'Etudes ijapodhani hivyo barabara, itakuwa na haki yakuwekea na kutoza ushuru kwa vyumba vya ushuru katika njia hizi, wakujipatia faida ili iweze kulipa gharama ya kuzijengea. Na njia zitakazofunguliwa hivyo zitashika, zaidi ya njia nyenyewe, upana wa mita ishirini kushoto na kulia kwa njia. Upana huu uwe baadhi ya ukomo, na utakuwa, kama njia nyenyewe, mali ya Comite d'Etudes. (2)Haki ya kutijara na wenyeji wamo katika nchi zao bila zuio. (3)Haki ya kulimia mashamba matupu: kuondoa miitu, kusanya mpira kihindi, sandarusi, nta, asali, na kwa jumla, vizao vyote vya tabia vinavyopatikana kule: kuvua samaki wamo majitoni, miitoni, au vijitoni, na kuendesha machimbo. Na yakuelewa kwamba Comiti ina uwezo wakutumiza haki zote mbali zimo kifungoni cha tatu hata kwa urefu wote wa nchi za wakuu wa Vivi.

  • Sharti la saba. - Wakuu wapa ahadi ya kuungisha nguvu zao pamoja na zile za Comite kufukuza mapigano yaweza kutokana na wapenyezi wa rangi yoyote. Wakuu, kwa kutojua kutia sahihi, wameweka alama zao hadhara ya mashahidi.
    ......Aug. Sparhawk
    ......John Kickbright
    ......Frank Mahoney
    ......Geoffrey

    Back to TOP


    "When the European powers (particularly Britain, Germany, France) 'scrambled' for parts of Africa in the last quarter of the nineteenth century, a common device for securing territories was by so-called 'treaty', often a ready-made blank document carried by colonial agents presented to local rulers for signing.... The following is such a document, with appropriate blank spaces, as employed by agents of the British Royal Niger Company. "- Prof. O'Brien

    Treaty of theBritish Royal Niger Company

    1.English version:

    Treaty of theBritish Royal Niger Company


    2.Kiswahili translation:

    Mapatano ya British Royal Niger Company

    Back to TOP


    I Previous page I Full page List I Next page

    © M. E. Kudrati, 2006:This document may be reproduced and redistributed, but only in its entirety and with full acknowledgement of its source and authorship
    m.kudrati.last updated 14/5/2008