PAGE 4
I Previous page I Full page List
I Next
page
![]() |
Construction manual for mediaeval Arabian sailing vessels/Kitabu kiarabu cha maunzi ya vyombo vya bahari vya zamani |
Kuona mafungo yahusiana
na Sultani ya Kilwa katika kitabu cha "Safari ya Ibn
Battuta" tumia kiungo / To view relevant passages on the Sultan of Kilwa itself
go to: Sultanate of Kilwa
".....Baadaye, nilivuka bahari kutoka mji wa Mogadishu, kuelekea nchi ya Sawahili, ili kusudia mji wa Kulwa katika nchi ya Zanuji. Tulifika hata mpaka kisiwa cha Mombasa, na hicho ni kisiwa kikubwa. Kati chake na nchi ya Sawahili ni muda wa siku mbili baharini, bila bara katikati. Hapa kisiwani pana migomba, milimau, na mindimu. Pia, pana matunda yaitwa 'jamuni' , ambayo yafanana na zeituni. Viini vya matunda haya ni vilevile kama zeituni, isipokuwa yayo na utamu wingi. Hayana mavuno kisiwani, na haya yavushwa kutoka Sawahili. Vyakula vyao, kwa zaidi, ni ndisi na samaki. Watu hawa ni wafuasi wa madhehebu ya Shafi, na wako watu wa dini na suluhu. Misikiti yao ya miti imejengwa na ustadi kweli. Mbele ya kila mlango wa milango ya msikiti kuna kisima kimoja na viwili, na kima cha visima hivi hufika dhiraa(1) moja au mbili. Maji ya kisima hunywa yenye vikombe vya mti ambavyo vimepenyezwa na fimbo nyembamba ya urefu wa dhiraa. Ardhi upande wa msikiti na kisima ni pana. Mtu yo yote akitaka kuingia msikitini huosha miguu yake miwili kabla kuingia ndani na, pia, mlangoni, kunako kipande kinene cha kumbi cha kupangusia miguu. Na yoyote akitaka kufanya wudhuu(2) hushika kikombe kati ya mapaja ya miguu yake na humiminia mkononi kutawadhuu. Pia, watu wote hutembea bila viatu.
Tulitulia kisiwani muda wa usiku na tulivuka bahari tena kwenda mji wa Kulwa. Huu ni mji mkubwa , wa pwani. Wenyeji wake ni wazanuji, weusi sana, na nyuso zao ziko zimechanjwa kama zile za watu wa Limi ya Janada. Baadhi ya matajiri walinijulisha kwamba mji wa Sofala ni muda wa mwezi nusu kutoka mji wa Kulwa, na kati ya Sofala na Yufa, kutoka nchi ya Limi, ni muda wa mwezi mzima. Tena, waleta dhahabu kutoka Yufa mpaka Sofala.
Mji wa Kulwa ni mji mzuri sana kuliko miingineyo, na umejengwa na ufundi, wote wa kutumiwa miti. Sakafu za nyumba zao zimetengenezwa na disi.(3) Mvua hapa hunyesha sana. Watu hawa ni wajitahidi sana kwa kuwa wakaaji wa bara moja inayoungamana na ile ya makafiri wa Zanuji. Na aghlabu ya watu hawa ni wanyofu na wenye dini, na wafuata madhehebu ya Shafi.".
Kitoleo hiki hasa ni chenye kitabu chake cha kiarabu kilichochapwa na Dar Beirut. Mfasiri ni mwandishi ameyotajwa chini.
Arabic text translated above:
.....من ذكر سلطان مقدشو
ثم ركبت البحر من مدينة مقدشو متوجها إلى بلاد السواحل قاصدا مدينة كلوا من بلاد الزنوج ، فوصلنا إلى جزيرة منبسى و هي جزيرة كبيرة بينها و بين ارض السواحل مسيرة يومين فى البحر ، و لا بر لها ، واشجارها الموز والليمون والأترج ، ولهم فاكهة يسمونها الجمون ، و هي شبه الزيتون ، و لها نوى كنواه إلا انها شديدة الحلاوة . ولا زرع عند اهل هذه الجزيرة و إنما يجلب إليهم من السواحل ، واكثر طعامهم الموز والسمك ، وهم شافعية المذهب اهل دين وعفاف وصلاح ، ومساجدهم من الخشب محكمة الاتقان ، وعلى كل باب من ابواب المساجدالبئر وا الثنتين ، وعمق ابارهم ذراع او ذراعان فيستقون منها الماء بقدح خشب قد غرز فيه عود رقيق طول الذراع ، والأرض حول البئر والمسجد مسطحة فمن اراد دخول المسجد غسل رجليه ودخل ، ويكون علي بابه قطعة حصير غليظ يمسح بها رجليه ، ومن اراد الوضوء امسك القدح بين فخذيه ، وصب علي يديه ويتوضا، و جميع اﻟنناس يمشون حفاة الأقدام .
وبتنا بهذه الجزيرة ليلة و ركبنا الحر إلى مدينة كلوا ، وهي مدينة عظيمة ساحلية اكثر اهلها الزنوج المستحكمو السواد ، ولهم شرطات في وجوههم كما هي في وجوه الليميين من جنادة ، وذكر لي بعض التجار ان مدينة سفالة على مسيرة نصف شهر من مدينة كلوا و ان بين سفالة و يوفى من بلاد الليميين مسيرة شهر ، ومن يوفى يؤتى بالتبر إلى سفالة .ومدينة كلوا من احسن المدن واتقنها عمارة وكلها بالخشب ، وسقف بيوتها الديس ، والأمطار بها كثيرة ، وهم اهل جهاد لأنهم في بر واحد متصل مع كفار الزنوج ، والغالب عليهم الدين والصلاح ، وهم شافعية المذهب.
For the sake of completeness the relevant excerpt from Gibb's translation is reproduced below :
"Then pursued our journey to Kulwá, which is a large town on the coast. The majority of its inhabitants are Zanj, with tattoo-marks on their faces. I was told by a merchant that the town of Sufála lies a fortnight's journey [south] from Kulwá, and that gold dust is brought to Sufála from Yúfí in the country of the Límís, which is a month's journey distant from it. Kulwá is a very fine and substantially built town, and all its buildings are of wood. Its inhabitants are constantly engaged in military expeditions, for their country is contiguous to the heathen Zanj."
Extract from Ibn Battūta, Travels in Asia and Africa 1325-1354 selected and translated by H. A. R. Gibb. Broadway Traveller's Series ( London : Routledge and Sons, 1939). Page 10.
Kuona mafungo yahusiana
na Sultani ya Kilwa katika kitabu cha "Safari ya Ibn
Battuta", tumia kiungo / To view relevant passages on the Sultan of Kilwa itself
go to: Sultanate of Kilwa
IBN BATUTA, ( أبو عبد الله محمد ابن بطوطة ), i.e. Abu Abdallah Mohammed, surnamed IBN BATUTA (b.1304-d.1377 AD), the greatest of Moslem travellers, was born at Tangier in 1304. He entered on his travels at twenty-one (1325) and closed them in 1355.
IBN BATUTA ( أبو عبد الله محمد ابن بطوطة ), Abu Abdullah Mohammed, aliyepata jina la Ibn Batuta( ٧٠٤ - ٧٧٩ ه ; k 1304-1377 .), msafiri maarufu Mwislamu, alizaliwa huko Tanjah , Magherebu, Afrika Kaskazini. Alianza safari zake umri wa ishirini na moja, mwaka wa ٧٢٥ ه , au 1325 k, na alimaliza zile mwaka wa ٧ ٥ ٦ ه, au 1355 k.
.For more biographical details on see linked article IBN BATUTA
Al-Jahiz, Abu Uthman Amr Ibn Bahr al-Kinani al-Fuqaimi al-Basri, (born in Basra, c. 781 ? December 868 or January 869) was a famous Arab scholar, believed to have been of East African descent.
Insha Juu ya waZanj.- kuhusiana na neno la 'Zanj'
Wote wanakubali kwamba hawana watu wakuza zaidi katika upaji kama Wazanji. Hawa wanao tabia ya asili kucheza na mpigo ya ngoma bila kufundishwa. Na hakuna waimbaji wazuri kuliko hao popote duniani, au watu wastadi zaidi, au wanao fasaha kuliko hao, au huwa wasiopenda kutumia maneno ya mashutumu. Nchi yoyote nyingine haina uwezo wa kushinda hao katika nguvu ya mwili wala ushupavu wake. Mmojawao atainua magogo makubwa na atabeba mizigo mizito yakupita uwezo wa mabedui au watu wa makabila mengine.Tena, wanao shujaa, bidii na karama ambazo ni maadili ya uungwana, pamoja na wema pia bila maelekeo ya ubaya. Hao huchekelea daima, watabasamu, na huwa wasio na uovu kabisa, na hizo ni alama za mwungwana.
Wazanji wasema kwa Waarabu: Nyinyi watu wajinga kweli kwa kuwa katika ujahili mlitufikiria sawa na nyinyi kuoana na wanawake Waarabu lakini, baada ya mwanzo wa hekima ya Islamu, mmeamua desturi hiyo kuwa mbaya. Hata sasa jangwa limejaa na Wazanji wameooa wanawake Waarabu, na wamekuwa maamiri na wafalme, na wamehifadhia haki zenu, na wamewekea nyinyi mahali pa amani juu ya maadui zenu.
Wazanji wasema kwamba Mungu hakuumba hao weusi kutopendezewa; ila ni mazingira yao yamefanya hao hivyo. Na ushahidi wake wazi ni kuishi makabila weusi miongoni mwa Waarabu, kama Banu Sulaim bin Mansur, tena watu wote ambao ni wakazi wa Harra, juu ya Banu Sulaim, ni weusi. Makabila hao wachukua watumwa kwa WaAshban, kuchunga wanyama wao, na kufanya kazi ya ujenzi wa njia za maji, kazi ya mikono, na kazi ya nyumbani, na mabibi wao ni waRumi; Hata hivyo, baada ya kadogo ya vizazi vitatu tu, watu wa Harra wote wamekuwa weusi. Kwa ajili ya jinsi inavyo patikana Harra, huwa paa, mbuni, madudu, mbwa mwitu, mbweha, kondoo, punda, farasi na ndege, na wote wanaoishi kule wako weusi. Ueupe na Ueusi wako kwa sababu ya mazingira, tabia na hali ya maji na ardhi, umbali wa jua, na ukali wa joto. Siyo swali la ubadiliko, au adhabu, au uharibifu, au neema ya Mungu. Tena, nchi ya Banu Sulaim aghlabu ni sawasawa na nchi ya WaTurki ambako ngamia, na wanyama wa mizigo na sura za nyinginezo zote zao zafanana ; yaani, vyote vyao vyaonekana viTuruki.
The Arabic text was not available to me. The above excerpt comes from the English paragraph published at Fordham Educational. To read it, use link provided; Tafsiri ya kitoleo hiki siyo kwa kiarabu, ambayo ni ya fungo katika kiingereza limelochapwa na Fordham educational. Kusoma kile tumia kiungo: al-Jahiz
For more information on al-Jahiz see:al-Jahiz
I Previous page I Full page List
I Next
page
© M. E. Kudrati, 2006:This document may be reproduced and redistributed, but only in its entirety and with full acknowledgement of its source and authorship |
---|