Bismillahir Rahmaanir Rahim

MUHTASARI WA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU KWA MADRASA NA SHULE ZA MSINGI

DARASA LA I
FANI MADA MADA NDOGO LENGO (MWANAFUNZI) MBINU ZA KUFUNDISHIA VIFAA/REJEA
QUR'AN Kusoma na Kuandika Kiarabu
  • Kutambua herufi za Kiarabu
  • Kusoma na kuandika herufi za Kiarabu
Aweze kusoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu
  • Mwalimu awaonyeshe na kuwatamkia wanafunzi herufi mojamoja Atumie picha na kadi.
  • Wanafunzi wamfuatishe Mwalimu kutamka herufi moja moja kwa wote kisha mmoja mmoja.
  • Wanafunzi wafanye mazoezi ya kuandika herufi moja moja katika ardhi, ubaoni, katika karatasi ngumu, n.k.
  • Mwalimu awatambulishe wanafunzi hatua kwa hatua alama za Irabu, tanwin na sakna na atoe mazoezi ya kutosha ya kusoma na kuandika herufi za Kiarabu zikiwa na alama hizo.
  • Mwalimu awaonyeshe herufi moja moja inavyokuwa ikiwa inaungwa mwanzoni, katikati na mwishoni mwa neno. Abainishe herufi zisizoungika na atoe mazoezi ya kutosha ya kusoma na kuandika.
  • Mwalimu awatambulishe wanafunzi alama za madda na shadda na zinavyotumika katika kusoma·
  • Mwalimu atoe mazoezi mengi ya kusoma na kuandika.
  • Ubao na chaki.
  • Kadi za herufi.
  • Kadi za maneno.
  • Mbao/ubao
  • Juzuu Amma
  • Kitabu cha I (IPC).
Kusoma Qur’an Kusoma kwa ufasaha sura ya: -
  • Al-Fatiha mpaka Al- A’laa
  • Kuhifadhi sura hizo
  • Kuandika
    • Al-Fatiha
    • Annas
    • Al-Falaq
    • Al-Ikhlas
  • Aweze kusoma Qur’an kwa ufasaha na kuhifadhi
  • Aweze kuandika Al-Fatiha, Annas, Alfalaq na al-Ikhlas
  • Mwalimu awasomee wanafunzi sura huku wakisikiliza kisha awaamuru kusoma katika kundi kisha mmoja mmoja.
  • Mwalimu awawezeshe wanafunzi kuhifadhi kwa kumfuatisha bila kuangalia kitabuni kwa kundi na kisha mmoja mmoja.
  • Mwalimu aandike ubaoni sura anayosomesha.
  • Mwalimu awaamuru wanafunzi kuandika al-Fatiha, annas, Al-Falaq na Ikhlas
  • Ubao na chaki.
  • Vibao vya wanafunzi.
  • Radio kaseti.
  • Kitabu cha I (IPC).
TAWHIID Kuwepo kwa Allah (S.W.). Allah ni muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Aweze kupambanua kuwepo kwa Allah (S. W.) kutokana na mazingira yake. Mwalimu awaulize wanafunzi maswali yatakayowapelekea kuyakinisha kuwepo kwa Allah (S. W.) kwa kutumia mazingira yao
  • Jua.
  • Mwezi.
  • Nyota.
  • Mawingu.
  • Kitabu cha I (IPC).
FIQ-H Nguzo za Uislamu
  • Kutoa Shahada
  • Kusimamisha Swala
  • Kutoa zaka
  • Kufunga Ramadhani
  • Kuhiji Makka kwa mwenye uwezo.
Aweze kutaja nguzo za Uislamu.
  • Mwalimu ataje nguzo tano – moja moja kisha wanafunzi wamfuatishie kwa kundi kisha mmoja mmoja. Atumie Hadithi “Buniyal Islamu alaa khamsin….”.
  • Wanafunzi wenyewe wataje nguzo tano katika kundi, kisha mmoja mmoja.
  • Picha ya nyumba
  • Yenye nguzo tano
  • Kitabu cha I (IPC)
Shahada
  • Kutamka na kuandika Shahada
  • Kutafsiri Shahada
Aweze kutamka na kuandika shahada
Aweze kutafsiri shahada
  • Mwalimu awawezeshe wanafunzi kutamka, kuandika na kutafsiri shahada mbili kwa kuwazoesha kutamka na kuandika shahada na tafsiri yake
  • Mwalimu awafahamishe wanafunzi kuwa maana ya shahada ni kufuata maamrisho na makatazo yote ya Allah (S.W.) na Mtume wake.
  • Mwalimu abainishe maamrisho na makatazo ya Allah na Mtume wake kulingana na umri wa wanafunzi.
Kitabu cha I (IPC)
Najsi na namna ya kujitwaha-risha
  • Vitu vilivyonajisi.
  • Namna ya kujitwaharisha kutokana na najisi.
  • Adabu za kwenda haja.
  • Kujitwaharisha baada ya kwenda haja
Aweze kujua najisi na namna ya kujitwaha-risha.
  • Mwalimu awatajie wanafunzi vitu vilivyo najisi – kimoja kimoja kulingana na uzoefu wa mazingira ya wanafunzi kama vile choo kikubwa na kidogo, damu, matapishi, mzoga, n.k.
  • Mwalimu awaelekeze wanafunzi kwa vitendo namna ya kuondoa najisi kwenye mwili, nguo, na mswala kisha awape wanafunzi mazoezi.
  • Mwalimu awaeleze wanafunzi kwa vitendo namna ya kujisaidia na kujitwaharisha kwa maji, mawe, karatasi, n.k.
  • Picha husika
  • Rejea kitabu cha I (IPC)
Kutawadha
  • Namna ya kutawadha
  • Yanayotengua udhu
  • Aweze kutawadha
  • Aweze kutaja yanayotengua udhu
  • Mwalimu awaelekeze wanafunzi kutawadha kwa vitendo na awape wanafunzi mazoezi ya kutawadha mmoja mmoja mbele ya darasa.
  • Aorodheshe ubaoni yale yanayotengua udhu na kuwataka wanafunzi wayarudie.
  • Ndoo ya maji
  • Makopo
  • Kata, n. k.
AKHLAQ Usafi
  • Kutwaharika na najisi nguoni na mwilini
  • Usafi wa mwili, kuoga, kuchana, kusuka, kukata kucha, n.k.
  • Usafi wa nguo: kufua, kupiga pasi,
  • Faida za usafi
Ajue kuwa usafi ni sehemu ya Uislamu
  • Kwa njia ya maelekezo na kumuuliza maswali mwalimu awafahamishe wanafunzi umuhimu na faida ya usafi.
  • Mwalimu awaelekeze wanafunzi kwa vitendo namna ya kupiga mswaki, kukoga, kuchana nywele, kufua, kupiga pasi, n. k.
  • Mwalimu kila mara awakague wanafunzi kwa usafi na unadhifu wa mwili na nguo.
  • Awafahamishe wanafunzi faida za usafi na hasara za uchafu.
  • Nguo chafu na safi.
  • Miswaki
  • Sabuni
  • Kitana
  • Kikata kucha n. k.
  • Rejea picha kitabu cha I (IPC)
Adabu za kula.
  • Kunawa kabla ya kuanza kula
  • Kuanza kula kwa Bismillah
  • Utulivu wakati wa kula na heshima kwa unaokula nao
  • Adabu za kula katika kundi
  • Kula kwa kiasi
  • Kumaliza kula kwa kumshukuru Allah (S. W.) na aliyeandaa chakula
  • Usafi baada ya kula
Aweze kula kwa kuzingatia Sunnah
  • Mwalimu awafahamishe wanafunzi vyakula vya halali akizingatia umri wao.
  • Kwa njia ya maelekezo na kuuliza maswali mwalimu awafahamishe wanafunzi vyakula vizuri vinavyokamilisha mlo na umuhimu wake katika mwili kulingana na umri wao
  • Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa vitendo namna ya kula kwa taratibu za Kiislamu
  • Chakula
  • Ndoo ya maji
  • Ndoo tupu
  • Glasi za maji, n.k.
  • Rejea picha kitabu cha I (IPC)
Michezo
  • Kucheza katika maeneo yanayokubalika.
  • Kujiepusha na michezo mibaya ya uharibifu.
  • Kucheza na watoto wenye maadili mema na kujiepusha na watoto wabaya.
Afahamu michazo na uchezaji unaokubaliana na maadili ya Kiislamu.
  • Awafahamishe wanafunzi michezo na uchezaji unaofaa na faida zake.
  • Awabainishie wanafunzi michezo mibaya na awatahadharishe wanafunzi kwa kuonyesha ubaya na hasara za michezo hiyo.
Kitabu cha I (IPC)
TAREKH Mitume wa Allah (S. W.)
  • Mitume 25 iliyotajwa katika Qur-an.
  • Mitume wote wamekuja kuufundisha Uislamu.
Afahamu kuwa Mitume wote wamekuja kufundisha Uislamu.
  • Mwalimu ataje majina ya Mitume 25 na kuwataka wanafunzi wamfuatishe.
  • Aorodheshe majina 25 kwenye ubao na kuwaamuru wanafunzi kuandika.
  • Asisitize kwa wanafunzi kuwa Mitume wote wamekuja kufundisha Uislamu.
Kitabu cha I (IPC)

Muhtasari kwa madarasa mengine

Home Darasa la Pili Darasa la Tatu Darasa la Nne Darasa la Tano Darasa la Sita Darasa la Saba

Muhtasari huu umetayarishwa na Islamic Propagation Centre, S. L. P. 55105, Dar es salaam, Tanzania