Bismillahir Rahmaanir Rahim

MUHTASARI WA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU KWA MADRASA NA SHULE ZA MSINGI

DARASA LA III
FANI MADA MADA NDOGO LENGO (MWANAFUNZI) MBINU ZA KUFUNDISHIA VIFAA/REJEA
QUR'AN Kusoma, kuhifadhi na kutoa ujumbe wa sura zilizochaguliwa
  • Hukumu za usomaji Qur-an.
  • Idh-hari, Id-gham, Ikh-fai, Iqlab.
  • Kuhifadhi sura zifuatazo: -
    Al-Mursalaat hadi Al-Jinn
  • Tafsiri ya sura zifuatazo: -
    An-Nabaa mpaka Atw-Twaariq.
  • Aweze kutambua na kutumia hukumu zote za Qur-an.
  • Ahifadhi Qur-an na aweze kutoa ujumbe sura zilizochaguliwa.
  • Mwalimu asome sura hizo kwa utaratibu na ufasaha.
  • Awape wanafunzi fursa ya kumfuatishia kwa darasa.
  • Awape wanafunzi kazi ya kuandika kila sura katika daftari na kuihifadhi.
  • Awape tafsiri na ujumbe wa sura hizo kwa maelezo na kuwaandikia ubaoni na kuwamuru kunakili.
  • Qur-an na tafsiri ya Al-Farsy.
  • Kitabu cha III (IPC)
TAWHIID Nguzo za Imani.
  • Katika Qur-an (2:285), n.k.
  • Katika Hadithi.
Afahamu nguzo za Imani kwa mpangilio.
  • Mwalimu asome aya na hadithi zinazobainisha nguzo za Imani na aziandike ubaoni na tafsiri yake.
  • Wanafunzi wasome kwa kumfuatisha mwalimu na waandike katika madaftari yao.
Kitabu cha III (IPC)
Kuwepo Allah (S. W.) Kuwepo kwa mwanaadamu ni dalili ya kuwapo Allah (S. W.) ukizingatia: -
  • Umbile lake.
  • Uhai wake.
  • Makuzi yake.
  • Usingizi wake.
  • Kufa kwake.
  • Tofauti ya lugha, rangi na makabila .
  • Aweze kumtambua Allah (S. W.) kutokana na mwanadamu.
  • Kumuwezesha kumuogopa na kumtii Allah (S. W.) inavyostahiki.
  • Mwalimu aulize maswali yote yanayowapelekea wanafunzi watambue kuwepo kwa Allah (S. W.) kutokana na nafsi ya mwanadamu.
  • Mwalimu kwa njia ya maswali na maelezo awafahamishe wanafunzi kuwa wanawajibika kumtii Allah (S. W.) na kumtumikia inavyostahiki kwa kufuata maamrisho yake na kuacha makatazo yake.
Kitabu cha III (IPC)
FIQH Sharti za Swala
  • Twahara.
  • Stara.
  • Kuchunga nyakati za Swala.
  • Kuelekea Qibla.
Aweze kutekeleza masharti yote ya Swala.
  • Mwalimu asomeshe kwa vitendo mipaka ya stara na namna ya kujisitiri.
  • Awape wanafunzi mazoezi ya kujisitiri.
  • Mwalimu afanye marudio ya darasa la pili katika Twahara, kuchunga wakati na kuelekea Qibla.
  • Nguo za stara kulingana na umri wa watoto.
  • Kitabu cha II (IPC)
  • Kitabu cha III (IPC)
Kuswali.
  • Nguzo na Sunna za Swala.
  • Yanayobatilisha Swala.
Aweze kuswali vilivyo.
  • Awatafsiriye kwa kuandika ubaoni visomo vyote vya Swala.
  • Awaonyeshe wanafunzi namna ya kuswali kwa unyenyekevu.
Kitabu cha III (IPC)
AKHLAQ Tabia njema.
  • Usafi.
  • Kuishi Kiislamu saa 24.
  • Awe msafi.
  • Awe na mwenendo wa Kiislamu.
  • Mwalimu asisitize kwa Aya na Hadithi umuhimu wa usafi.
  • Awaelekeze wanafunzi namna watakavyoweza kuishi Kiislamu katika saa 24 kwa kurejea Hadithi sahihi.
Kitabu cha III (IPC)
TAREKH Historia ya Uislam wakati wa Mtume Muhammad (S. A. W.)
  • Kupewa Utume.
  • Wahy wa kwanza na ujumbe wake.
  • Kubalighisha Uislamu.
  • Upinzani alioupata Makkah.
  • Mateso kwa Waislamu.
  • Kuhamia Madina.
Aweze kueleza namna Mtume (S. A. W.) alivyoanza kuhuisha Uislamu na mafunzo tunayopata kutokana na kipindi hiki cha historia.
  • Mwalimu awahadhithie wanafunzi historia ya Mtume (S. A. W.) tangu kupewa Utume mpaka kuhamia Madinah hatua kwa hatua.
  • Mwalimu abainishe mafunzo yanayopatikana katika kila hatua kulingana na umri wa wanafunzi.
Kitabu cha III (IPC)

Muhtasari kwa madarasa mengine

Home Darasa la Kwanza Darasa la Pili Darasa la Nne Darasa la Tano Darasa la Sita Darasa la Saba

Muhtasari huu umetayarishwa na Islamic Propagation Centre, S. L. P. 55105, Dar es salaam, Tanzania