DARASA LA IV
FANI |
MADA |
MADA NDOGO |
LENGO (MWANAFUNZI) |
MBINU ZA KUFUNDISHIA |
VIFAA/REJEA |
QUR'AN |
Kusoma. |
- Ahkai – marudio darasa la III
- Kuhifadhi na tafsiri ya sura zifuatazo: -
Tafsiri ya Surat Al-Mursalaat, al-Jinn
- Ujumbe wa sura zifuatazo: -
Al-Fatiha mpaka Al-zilzal
|
- Aweze kusoma Qur-an vilivyo.
- Ahifadhi na kutafsiri Qur-an na apate ujumbe uliomo na aweze kuufuata
|
- Mwalimu asome kila sura mbele ya darasa kwa utaratibu na ufasaha na awape wanafunzi fursa ya kumfuatisha.
- Wanafunzi waandike kila sura katika madaftari yao na kuhifadhi.
- Atoe tafsiri na ujumbe wa kila sura na kuwapa wanafunzi mazoezi ya kutafsiri na kubainisha ujumbe.
- Aandike tafsiri na ujumbe wa kila sura ubaoni na wanafunzi wanakili madaftarini.
|
Kitabu cha IV (IPC) |
TAWHIID |
Kumuamini Allah (S. W.) |
- Sifa za Allah (S. W.) katika Qur-an na Hadith.
- Matumizi ya sifa za Allah katika kuomba dua.
- Maana ya kumuamini Allah (S. W.)
|
Aweze kumuamini Allah (S. W.) ipasavyo na asimshirikishe na chochote. |
- Mwalimu awasomee na kuwaandikia ubaoni majina 99 ya Allah (S. W.) kama yalivyobainishwa katika Hadith na kuwaamuru waandike.
- Kisha arejee sura na aya mbalimbali zinazotaja baadhi ya sifa za Allah kwa mfululizo kama aya (2:225), (57:1-6), (59:22-24), (112:1-4)
|
Kitabu cha IV (IPC) |
FIQ-H |
Kusimamisha Swala |
- Kujitwaharisha kwa tayammamu.
- Maana ya kusimamisha Swala.
- Sijidatis-Sahau.
- Sijida-tilawat.
- Unyenyekevu katika Swala.
- Swala ya jamaa.
- Dua na dhikiri baada ya Swala.
|
- Aweze kutayamamu.
- Aweze kueleza maana ya kusimamisha Swala.
-
- Aweze kuleta sijidatis –Sahau na Tilawat.
- Aweze kusimamisha Swala ya jamaa.
- Aweze kuleta dua na dhikiri baada ya Swala.
|
- Mwalimu aelezee kinadharia na matendo namna ya kutayamamu.
- Awaelekeze wanafunzi kwa matendo namna ya kuleta sijidatis-sahu na tilawat.
- Awaelekeze kwa matendo namna ya kusimama kwenye Swala ya jamaa.
- Mwalimu awaelekeze wanafunzi namna ya kufanya ili waweze kunyenyekea katika Swala.
- Awasomee dua na dhikiri na kuwaimbisha na kisha kuwaandikia ubaoni na kuwaamuru wanakili.
|
Kitabu cha IV (IPC) |
Zakat |
- Maana ya Zakat.
- Wanaopaswa kutoa Zakat.
- Vitu vinavyotolewa Zakat na viwango vyake.
- Wanaostahiki kupewa Zakat.
|
Aweze kueleza maana ya Zakat, utoaji wake na mgawanyo wake. |
Awafahamishe maana ya Zakat, wanaopaswa kutoa, vitu vinavyotolewa Zakat na viwango vyake na wanaostahili kupewa Zakat kwa kutumia aya za Qur-an na Hadithi. |
Kitabu cha IV (IPC) |
Funga ya Ramadhani. |
- Amri ya funga ya Ramadhani (2:183).
- Wanaolazimika kufunga.
- Wanaoruhusiwa kufunga.
- Wanaoruhusiwa kula na kulipa baadaye.
- Nia ya kufunga.
- Maana ya kufunga.
- Tabia anayotakiwa awe nayo mfungaji.
- Yanayobatilisha funga.
|
Aweze kufunga ipasavyo. |
- Mwalimu asome na kuandika ubaoni aya (2:183) juu ya funga.
- Mwalimu abainishe kwa maelezo na kuandika ubaoni wanaolazimika kufunga, wenye kuruhusiwa na kulipa baadaye kwa kurejea Qur-an (2:184-185), namna ya kufunga, tabia ya mfungaji na yanayobatilisha funga.
|
Kitabu cha IV (IPC). |
AKHLAQ |
Mavazi ya Kiislamu |
- Lengo la vazi (7:26-27).
- Vazi la mwanaume na mwanamke.
- Faida ya Hijab (33:59).
|
Aweze kujisitiri Kiislamu. |
- Mwalimu awafahamishe wanafunzi lengo la vazi kwa kurejea Qur-an (7:26-27) na asisitize faida na umuhimu wa kujisitiri – (33:59).
- Mwalimu aonyeshe kwa vielelezo namna ya kujisitiri Kiislamu kwa wanaume na wanawake.
|
Kitabu cha IV (IPC) |
Michezo |
- Michezo inayoruhusiwa katika Uislamu.
- Michezo iliyoharamishwa.
- Michezo ya laghwi.
|
Aweze kushiriki katika michezo iliyoruhusiwa na kujiepusha na michezo haramu na ile ya laghwi. |
- Mwalimu abainishe michezo inayokubalika katika Uislamu.
- Mwalimu aainishe michezo haramu na michezo ya Laghwi.
- Mwalimu asisitize umuhimu wa kushiriki katika michezo yenye manufaa kwa vijana.
|
Kitabu cha IV (IPC). |
TAREKH |
Historia ya Uislam wakati wa Mtume (S. A. W) kipindi cha Madinah. |
- Mtume (S. A. W) kuunda umma wa Kiislamu.
- Upinzani Dhidi ya Dola ya Kiislamu.
- Mkataba wa Hudaibiya na matunda yake.
- Kukombolewa Makkah.
- Msafara wa Tabuuk.
- Kusilimu Waislamu makundi kwa makundi.
- Hija ya kuaga.
- Kutawafu Mtume.
|
Aweze kueleza namna Mtume (S. A. W) alivyosimamisha Dola ya Kiislamu Madinah, namna alivyoihami na kuufanya Uislamu kuwa juu ya dini zote. |
- Mwalimu aeleze hatua kwa hatua namna Mtume (S. A. W) alivyosimamisha Dola ya Kiislamu Madinah na kuufanya Uislamu kuwa juu ya Dini zote.
- Mwalimu atoe mazingatio tunayopata hivi leo.
|
Kitabu cha IV (IPC) |
Muhtasari huu umetayarishwa na Islamic Propagation Centre, S. L. P. 55105, Dar es salaam, Tanzania