DARASA LA II
FANI |
MADA |
MADA NDOGO |
LENGO (MWANAFUNZI) |
MBINU ZA KUFUNDISHIA |
VIFAA/REJEA |
QUR’AN |
Kusoma na kuandika |
- Kusoma na kuhifadhi sura zifuatazo: -
Atwaariq hadi An-Nabaa
- Kutoa tafsiri ya sura zifuatazo: -
Al-Fatiha hadi Al-Aqlaa
|
- Aweze kusoma Qur-an kwa ufasaha na kuhifadhi
- Aweze kutoa ujumbe wa Suratil Fatihat hadi Al-Ikhlas
|
- Mwalimu awasomee wanafunzi kwa utaratibu na ufasaha kisha awape nafasi ya kusoma wote kisha mmoja mmoja.
- Mwalimu awahifadhishe wanafunzi kwa kuwakaririsha na kuwaamuru waandike sura katika vibao (au madaftari).
- Mwalimu awafahamishe kwa maelezo na kuwaandikia tafsiri na ujumbe wa sura zilizochaguliwa.
|
- Vibao
- Kitabu cha II (IPC)
|
TAWHIID |
Kuwepo kwa Allah (S. W.) |
Allah (S. W.) ni Chanzo cha Uhai |
Aweze kutambua kuwa Allah (S. W.) ndiye chanzo cha uhai kutokana na mazingira yake. |
Mwalimu awaulize wanafunzi maswali yatakayowapelekea kuyakinisha kuwa chanzo cha uhai ni Allah (S. W.). |
- Mimea
- Wanyama
- Mimea ya Plastiki
- Vinyago, n.k
- Rejea picha kitabu cha II (IPC).
|
Allah (S. W.) anastahiki kutiiwa na kushukuriwa. |
Aweze kutambua kuwa Allah (S. W.) ni wakutiiwa na kuogopwa kuliko yeyote yule. |
Kwa njia ya kuuliza maswali, mwalimu awafahamishe wanafunzi kuwa wanalazimika kumuogopa na kumtii Allah (S. W.) kwa unyenyekevu kwa kufuata maamrisho yake kama vile kuswali, kuwatii wazazi, n.k. na kutekeleza makatazo yake kama vile kusema uwongo, kuiba, n.k. |
Kitabu cha II (IPC) |
FIQ-H |
Nguzo za Uislamu |
Hadithi juu ya nguzo tano za Uislamu |
Aweze kuorodhesha nguzo tano za Uislamu |
Kwa maelezo na kuandika, mwalimu awawezeshe wanafunzi kuisoma na kutafsiri Hadithi hii kisha awaamuru wanafunzi kuiandika pamoja na tafsiri yake. |
Kitabu cha II (IPC) |
Shahada |
Shahada mbili |
Aweze kutoa shahada mbili |
Mwalimu aeleze kwa kutumia mfano wa jengo lenye nguzo tano katika kuonyesha, maana halisi ya Hadithi hii. |
Kitabu cha II (IPC) |
Twahara |
- Maji ya kujitwaharishia
- Kujitwaharisha kutokana na najisi kubwa
- Kutawadha na dua baada ya kutawadha
|
Aweze kujitwaharisha inavyostahiki |
- Mwalimu awawezeshe wanafunzi kutwaharisha najisi ya mbwa na nguruwe kwa maelezo na vitendo na kutoa mazoezi katika vikundi na mbele ya darasa.
- Mwalimu awahifadhishe wanafunzi dua zilizotajwa na tafsiri zake kwa njia ya kuwasomea na kuandika.
|
- Mchanga
- Ndoo ya maji
- Kata la maji
- Nguo, n.k.
- Miswala
- Kitabu cha II (IPC)
|
Kuswali |
- Kuadhini
- Kukimu
- Nguzo na Sunnah za Swala
|
Aweze kuswali |
- Mwalimu aelekeze kuswali kwa vitendo na awafahamishe visomo vyote vya swala kwa kuandika na kuwahifadhisha
- Mwalimu awape wanafunzi mazoezi ya kuswali mbele ya darasa.
|
Kitabu cha II (IPC) |
AKHLAQ |
Usafi. |
- Aya na hadithi mbili zinazosisitiza usafi.
- Usafi wa mwili, nguo na mazingira.
|
Aweze kuwa msafi wa mwili, nguo na mazingira. |
Mwalimu aeleze na aulize maswali yatakayowapelekea wanafunzi kufahamu faida na hasara ya uchafu wa mwili, nguo na mazingira. |
Kitabu cha II (IPC) |
Tabia njema. |
- Kumbuka Allah (S. W.) kila wakati.
- Kuwahurumia wagonjwa, wadogo, n.k.
- Kushirikiana katika mambo mema.
- Utii kwa wazazi na viongozi, wakubwa kiumri katika hadhi.
- Maamkizi.
|
Awe na mwenendo wa Kiislamu. |
- Mwalimu aeleze na kuorodhesha dua na maneno yatakayowapelekea kumkumbuka Allah (S. W.) kila mara.
- Kuwaonyesha wanafunzi umuhimu wa kuwa na huruma, kuwatii wazazi na wakubwa.
- Awaeleze wanafunzi namna na adabu ya kusalimiana Kiislamu.
|
Kitabu cha II (IPC) |
TAREKH |
Mtume Muhammad (S. A. W) |
- Mtume Muhammad (S. A. W) ni Mtume wa mwisho.
- Kuzaliwa kwake.
- Nasaba yake.
- Malezi na makuzi yake.
- Tabia yake katika utoto na ujana.
- Familia yake (mke na watoto).
- Mwenendo wake alipokaribia kupewa Utume.
- Kupata Utume.
|
Aweze kuelezea historia ya Mtume katika katika kipindi hiki na mafunzo yatokanayo. |
Mwalimu awasimulie wanafunzi historia ya Mtume (S. A. W) tangu utotoni mwake hadi kupewa UtumeMwalimu aainishe mafunzo yatokanayo na historia hiyo. |
Kitabu cha II (IPC) |
Muhtasari huu umetayarishwa na Islamic Propagation Centre, S. L. P. 55105, Dar es salaam, Tanzania