Bismillahir Rahmaanir Rahim

MUHTASARI WA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU KWA MADRASA NA SHULE ZA MSINGI

DARASA LA VI
FANI MADA MADA NDOGO LENGO (MWANAFUNZI) MBINU ZA KUFUNDISHIA VIFAA/REJEA
QUR'AN Kusoma, kutafsiri na kutoa ujumbe wa sura zilizochaguliwa Kusoma na kutafsiri sura zifuatazo: -
  • At-Taghaabun hadi Al-Mujadillah.
  • Tafsiri na ujumbe wa Atw-Taariq hadi An-Nabaa
Ahifadhi na kutafsiri Qur-an na apate ujumbe uliomo na kuufuata
  • Mwalimu asome kila sura huku wanafunzi wakifuatisha kisha wanafunzi waandike sura hizo na kuzihifadhi.
  • Atoe tafsiri na ujumbe wa kila sura na awape wanafunzi mazoezi ya kutafsiri na kubainisha ujumbe. Kisha aandike ubaoni tafsiri ya kila sura na ujumbe wake na wanafunzi wanakili madaftarini mwao.
Kitabu cha VI (IPC)
HADITH Sunnah na Hadithi
  • Maana ya sunna.
  • Maana ya Hadithi.
  • Nafasi ya sunna katika Uislamu.
Atambue umuhimu wa Sunna katika uislamu. Mwalimu awafahamishe wanafunzi maana ya sunnah, maana ya hadithi na nafasi ya sunna katika Uislamu kwa njia ya maelezo na kuandika ubaoni. Kitabu cha VI (IPC)
TAWHIID Kuamini Mitume wa Allah (S. W.)
  • Umuhimu wa kuamini Mitume wa Allah (S. W.)
  • Sifa za Mitume wa Allah (S. W.)
  • Kazi za Mitume wa Allah (S. W.)
  • Ujumbe wa Mitume wa Allah (S. W.)
  • Maana ya kuamini Mitume katika maisha ya kila siku.
Atambue athari ya kuamini Mitume katika maisha ya kila siku.
  • Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa maelezo na kuandika ubaoni umuhimu wa kuamini Mitume wa Allah (S. W.), sifa za Mitume, kazi za Mitume, Ujumbe wa Mitume.
  • Abainishe tabia ya muumini wa kweli na Mitume wa Allah (S. W.)
Kitabu cha VI (IPC)
Kuamini siku ya Mwisho.
  • Umuhimu wa kuamini siku ya mwisho.
  • Ni ipi siku ya mwisho.
  • Athari ya kuamini siku ya mwisho katika maisha ya kila siku.
Aweze kuishi kama muumini wa kweli wa siku ya malipo.
  • Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa maelezo na kuandika ubaoni umuhimu wa kuamini siku ya malipo, mazingira ya akhera kwa mujibu wa Qur-an na Hadith.
  • Kisha abainishe na asisitize tabia ya muumini wa kweli wa siku ya malipo.
Kitabu cha VI (IPC)
Kuamini Qadar ya Allah (S. W.)
  • Nini Qadar.
  • Umuhimu wa kuamini Qadar.
  • Athari ya kuamini Qadar.
Aweze kutambua maana ya kuamini Qadar katika maisha ya kila siku. Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa maelezo na kuandika ubaoni umuhimu wa kuamini Qadar katika maisha ya kila siku. Kitabu cha VI (IPC)
FIQH Hija
  • Maana ya Hija.
  • Tofauti ya Hija na Umra.
  • Anayelazimika kuhiji.
  • Matendo ya Ibada ya Hija.
  • Idil-Hajj na Sunnah ya kuchinja.
  • Lengo la Hija
Aweze kulieleza lengo la Hija na linavyofikiwa.
  • Mwalimu awafahamishe wanafunzi kwa maelezo na kuandika ubaoni, maana ya Hija, tofauti ya Hija na Umra, wanaolazimika kuhiji.
  • Kwa kutumia vielelezo awafahamishe wanafunzi namna ya kutekeleza ibada ya Hija, Idil-Hajj na Sunnah ya kuchinja.
  • Kwa kurejea matendo ya Hija awaonyeshe lengo la Hija linavyofikiwa.
Kitabu cha VI (IPC)
AKHLAQ Kusimamisha Haki.
  • Haki za Allah.
  • Haki za mwili.
  • Haki za mume na mke.
  • Haki za wazazi.
  • Haki za watoto
  • Haki za udugu na jamaa.
  • Haki za masikini, yatima, n.k.
  • Haki za Kiongozi.
  • Haki za Waislamu (raia).
  • Haki za binadamu.
  • Haki za wanyama, n.k.
Aweze kusimamisha Haki ipasavyo. Mwalimu awafahamishe wanafunzi Haki zote kwa kurejea Qur-an na Hadithi. Kitabu cha VI (IPC)
TAREKH Historia ya Uislam kipindi cha Makhalifa.
  • Abubakar (R. A)
  • Ummar (R. A)
  • Uthman (R. A)
  • Aliy (R. A)
Aweze kutoa hoja kuwa wajibu wa kusimamisha Dola ya Kiislamu umebakia kwa Waislamu hata baada ya kutawafu Mtume (S. A. W) Mwalimu asimulie kwa muhutasari namna Makhalifa wa Mtume (S. A. W) walivyotekeleza wajibu wao katika kuendesha Dola ya Kiislamu – Matatizo yaliyowakuta na namna walivyoyatatua. Kitabu cha VI (IPC)

Muhtasari kwa madarasa mengine

Home Darasa la Kwanza Darasa la Pili Darasa la Tatu Darasa la Nne Darasa la Tano Darasa la Saba

Muhtasari huu umetayarishwa na Islamic Propagation Centre, S. L. P. 55105, Dar es salaam, Tanzania