DARASA LA VII
| FANI |
MADA |
MADA NDOGO |
LENGO (MWANAFUNZI) |
MBINU ZA KUFUNDISHIA |
VIFAA/REJEA |
| QUR-AN |
Kusoma, kutafsiri na kuhifadhi. |
Kuhifadhi, kutafsiri sura au aya zifuatazo (Rejea Msahafu wa tafsiri): -
- Al-Baqara (2); 1-20, 183-188, 254-257, 284-286.
- Al-Imraan (3): 102-120, 190-200.
- An-Nisaa (4): 11-13.
- Al-Kahf(18): 1-31.
- Al-Muuminuun (23): 63-77.
- Luqman (31): 1-34.
- Ahzaab (33): 9-27.
- Haamiim Sajda (41).
- Al-Fatih (48): Yote.
|
Ahifadhi Qur-an, ajue ujumbe unaopatikana na awe tayari kuufuata. |
- Mwalimu asome kila sura huku wanafunzi wakimfuatisha kisha waandike sura au aya hizo madaftarini mwao na kuzihifadhi.
- Atoe tafsiri na ujumbe wa kila sura au aya kwa maelezo na kuandika ubaoni, kisha wanafunzi wanakili madaftarini mwao.
|
Kitabu cha VII (IPC). |
| HADITH |
Historia ya kukusanywa na kuhifadhiwa Hadith. |
- Kuhifadhiwa Hadithi.
- Historia ya uandishi wa Hadithi wakati wa Mtume
- Maswahaba.
- Taabiina.
- Tabii-Taabiina.
|
Aweze kueleza vilivyopatikana vitabu vya Hadithi Sahihi. |
- Mwalimu awafahamishe wanafunzi utaratibu uliotumika katika kuhifadhi Hadithi.
- Aeleze kwa muhtasari historia ya kuandikwa Hadithi kwa kuwataja Maimam walioshughulika na uandishi wa Hadithi na historia ya maisha yao kwa ufupi.
|
Kitabu cha VII (IPC) |
| Uchambuzi wa Hadithi. |
- Migawanyiko ya Hadithi.
- Vigezo vya Hadith Sahihi.
|
Aweze kutambua Hadithi Sahihi. |
- Mwalimu abainishe migawanyiko yote ya Hadith kama vile Nabawiy, Qudus, Sahihi, Hasan, Dhaifu, Maudhuu, n.k.
- Abainishe vigezo vyote vya Hadithi sahihi kwa kuzingatia Matini na Isnad ya Hadithi.
Kitabu cha VII (IPC) |
|
| TAWHIID |
Imani ya Kiislamu |
- Maana ya kuamini katika Uislamu.
- Muumini wa kweli.
- Maana ya kuamini kila kipengele cha nguzo za Imani.
|
Aweze kuwa muumini wa kweli. |
- Mwalimu aeleze maana ya imani kilugha na kiistilah.
- Kwa kurejea Hadithi abainishe vipengele sita vya nguzo za Imani na wanafunzi wanukuu Hadithi hiyo.
- Kwa kurejea Qur-an na Hadith aonyeshe ni ipi tabia ya muumini wa kweli wa kila kipengele cha Imani.
|
Kitabu cha VII (IPC) |
| FIQ-H |
Maana ya Dini. |
- Maana ya dini katika Uislamu.
- Kila mtu anayo dini.
- Hakuna maisha ya dini na dunia.
- Aina kuu za dini.
|
Aweze kueleza maana ya dini na kuwa kila mtu ana dini. |
- Awafahamishe wanafunzi maana ya dini kwa kurejea Qur-an na Hadithi na abainishe kutokana na maana hiyo kuwa kila mwanaadamu anafuata dini moja au nyingine.
- Kwa kutumia Qur-an aonyeshe kuwa Ukafiri, Ushirikina, Utawa na Uislamu ni dini.
- Asisitize kuwa kwa mujibu wa Qur-an Uislamu ndio dini sahihi.
|
Kitabu cha VII (IPC) |
| Ibada. |
- Maana ya Ibada.
- Lengo la kuumbwa binadamu.
- Lengo la nguzo za Uislamu kwa ujumla.
|
Aweze kueleza maana ya Ibada katika Uislamu. |
- Awafahamishe wanafunzi kwa maelezo na kuandika ubaoni maana ya Ibada, lengo la kuumbwa mwanaadamu na lengo la kusimamisha nguzo tano za Uislamu.
- Asisitize kuwa Muislamu anatakiwa awe katika Ibada katika kila kipengele cha maisha yake na aonyeshe ni vipi mtu atakuwa katika Ibada muda wote wa saa 24.
|
Kitabu cha VII (IPC) |
| Twahara. |
- Hadathi.
- Aina za Hadathi.
- Kujitwaharisha na Hadathi.
|
Aweze kujitwaharisha vilivyo. |
Awafahamishe wanafunzi maana ya Hadathi, aina za Hadathi na namna ya kujitwaharisha kutokana na Hadathi kwa matendo |
Kitabu cha VII (IPC) |
| Maiti ya Kiislam. |
- Yaliyolazima kufanyiwa maiti.
- Kuosha.
- Kukafini.
- Kuswali.
- Kuzika.
|
Aweze kutekeleza mambo yote muhimu yanayostahiki kufanyiwa maiti ya Kiislamu. |
Awaonyeshe wanafunzi kwa vitendo namna ya kuosha maiti, kumvesha sanda, kumswalia na kumzika. |
Kitabu cha VII (IPC) |
| AKHLAQ |
Mwenendo wa Muislamu katika Qur-an. |
- Kumkumbuka Allah kila wakati.
- Kumuogopa Allah ipasavyo.
|
Awe na mwenendo wa Kiislamu. |
- Mwalimu aonyeshe ni vipi mtu ataweza kumkumbuka alla (s.a.w) katika masaa 24 kwa kurejea dua na dhikiri za Mtume (S. A. W) alizozileta katika nyakati mbalimbali katika saa 24.
- Asisitize umuhimu wa kumwogopa Allah (S. W.) na kumtegemea kila wakati.
|
Kitabu cha VII (IPC) |
Tabia ya Muumini katika Qur-an. |
- Nani Muumini.
- (8:2-4), (49:15)
- (23:1-11),
- (70:19-35)
- (25:63-77) n.k.
|
Awe na mwenendo wa Kiislamu. |
Mwalimu azipitie aya zilizochaguliwa na kudhihirisha vipengele vyenye tabia njema vilivyo bainishwa humo. |
Kitabu cha VII (IPC) |
| TAREKH |
Historia ya Uislamu baada ya Khalifa wanne mpaka hivi leo. |
- Yaliyopelekea kuvunjika kwa Dola ya Kiislamu.
- Mgawanyiko wa Waislamu na chanzo cha kundi la Shia.
- Kuibuka kwa kundi la Sunni.
- Juhudi za watu binafsi na vikundi katika kuhuisha Uislamu.
- Uislamu ulivyoingia Afrika Mashariki.
- Historia fupi ya Uislamu hapa Tanzania.
|
Awe na ari ya kusimamisha Dola ya Kiislamu katika jamii. |
Mwalimu kwa muhtasari aeleze historia ya Uislamu baada ya Khalifa wanne mpaka hivi leo akizingatia matukio muhimu na mafundisho yanayopatikana humo. |
Kitabu cha VII (IPC) |
Muhtasari huu umetayarishwa na Islamic Propagation Centre, S. L. P. 55105, Dar es salaam, Tanzania