MUHTASARI huu umezingatia yale anayotakiwa ayafahamu kijana wa Kiislamu anapokuwa katika Madrasa na shule ya Msingi kuanzia darasa la I hadi la VII Muhtasari huu umegawanywa katika fani zifuatazo: -
- Qur’an
- Hadith
- Tawhiid
- Fiq-h
- Akhlaq
- Tarekh
Kila fani imegawanywa katika mada na mada ndogo. Lengo la kila mada limebainishwa pamoja na mbinu za kufundishia ili kufikia lengo. Mbinu za kufundishia zilizobainishwa katika muhutasari huu ni kwa ufupi sana. |
Mwanafunzi atakapomaliza mafunzo haya anatarajiwa: -
- Aweze kusoma Qur’an Kama inavyotakiwa.
- Aweze kuhifadhi sura zote za juzuu tatu za mwisho, yaani Juzuu ya 28 hadi Juzuu ya 30 na sura nyinginezo kama zilivyoainishwa katika muhutasari huu.
- Aweze kutafsiri na kutoa ujumbe wa sura zote za Juzuu Amma
- Kujengeka kiimani na kuishi ndani ya mwenendo wa Kiislamu unaobainishwa katika Qur’an Na Hadithi Sahihi.
- Aweze kusimamisha nguzo za Uislamu vilivyo na kufikia lengo lililokusudiwa.
- Awe na ari ya kuusimamisha na kuuhami Uislamu katika jamii.
|